Pongezi serikali kutumia Ziwa Victoria kusambaza maji nchini

TUNAPONGEZA hatua ya serikali kuendelea kutumia maji ya Ziwa Victoria kwa ustawi wa wananchi katika kuboresha huduma za maji safi na salama.

Pongezi zetu zinarejelea mradi wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 55 (Sh bilioni 134.76) wa maji kwa wananchi wa Biharamulo utakaotekelezwa na Serikali ya Hungary kwa ajili ya wananchi wa Biharamulo mkoani Kagera.

Hii ni hatua muhimu inayoonesha dhamira ya serikali kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za maji.

Uendelezaji wa miradi hii ya kutumia maji ya Ziwa Victoria, una manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuboresha afya za wananchi, kupunguza magonjwa yanayohusiana na ukosefu wa maji safi na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta ya kilimo, viwanda na biashara.

SOMA: Maji Ziwa Victoria kufikishwa Dodoma

Imeshuhudiwa miradi mingine iliyokwishatekelezwa na mingine ikiwa katika mipango kutumia maji hayo ya Ziwa Victoria.

Mathalani, wakazi wa Kahama mkoani Shinyanga wameshanufaika na maji kutoka ziwa hilo kupitia mradi uliotekelezwa na serikali. Vilevile mikoa ya Singida na Dodoma ipo kwenye mipango ya serikali ya kupokea maji kutoka ziwa hilo.

Miradi hii itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la uhaba wa maji; itaboresha huduma na kuleta maendeleo ya kijamii.

Imeelezwa kwamba Hungary wana teknolojia nzuri ya maji zikiwemo za kuyasafirisha kwa masafa marefu na mbinu nyingine za kisasa. Hii ni hatua muhimu itakayoimarisha usalama wa maji nchini.

Ni ukweli ulio wazi kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imeonesha dhamira kubwa ya kuboresha huduma za kijamii zikiwemo huduma za maji kama ambavyo taarifa mbalimbali zinaonesha.

Kupitia sera na mikakati madhubuti, serikali imetekeleza jukumu la kucukua hatua za kuhakikisha huduma za maji zinapatikana kila mahali kurahisisha maisha ya wananchi ikizingatiwa kwamba maji ni uhai.

Jitihada hizi zinatoa ahadi ya kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku zikiimarisha ushirikiano wa kimataifa
kwa kutumia teknolojia za kisasa na fedha za uwekezaji zenye masharti nafuu.

Kwa ujumla, hatua ya uwekeza katika mradi huu unaoihusisha Hungary, inatoa matumaini kwa wananchi wa Biharamulo na mikoa mingine kwani ni mwanga mpya wa maendeleo na ustawi wa maisha ya watu.

Hatua hii inadhihirisha dhamira ya serikali kupitia mkopo huo wa miaka 18 usio na riba kujenga jamii yenye afya njema, maendeleo endelevu, na ustawi wa wote.

Tunasisitiza miradi ya namna hii iendelezwe ili kuhakikisha taifa linapata faida kubwa zaidi kutoka katika rasilimali zake za maji katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Ni matarajio yetu kwamba serikali itaendelea kutumia fursa ya rasilimali hii ya Ziwa Victoria kusambaza huduma
ya maji katika maeneo mbalimbali nchini kadiri ya mahitaji ya jamii.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ RFoRr Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button