Vyuo vikuu vyakumbushwa mabadiliko tabianchi

MOROGORO: KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo amevitaka vyuo vikuu nchini kuunganisha nguvu katika kufanya tafiti za pamoja ili kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa za kupata majawabu yakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Profesa Nombo, alitoa rai mkoani Morogoro wakati akifungua mkutano wa Pili wa Kisayansi wa Muungano wa Vyuo Vikuu Vitano nchini.

Muungano wa huo wa vyuo vikuu vitano unaundwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU), Taasisi ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika (NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Simon Fraser (SFU) kilichopo nchini Canada.

Katibu mkuu wa wizara hiyo amesema ushirikiano wa Vyuo vikuu ni chanzo cha maarifa, ubunifu wa suluhisho na nguzo ya kulinda vizazi vijavyo kwa maendeleo endelevu.

Profesa Nombo amesema mkutano huo ni muhimu kwa kuwa jamii zinakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula, mifumo dhaifu ya afya na ukosefu wa usawa wa kijamii.

“Nichukue mfano ,ukame wa hivi karibuni nchini Tanzania umepunguza mavuno kwa kiwango kikubwa na kuonesha haja ya kuimarisha kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi, aidha janga la COVID -19 limetufundisha umuhimu wa kuwa na mifumo imara ya afya,” amesma Profesa Nombo.

Profesa Nombo amesisitiza nafasi ya Muungano wa vyuo hivyo katika kushirikiana na kubadilishana rasilimali, vifaa vya utafiti na wataalamu.

“ Kwa kupitia ushirikiano huu ubora wa tafiti unaweza kuongezeka, sera zikaimarishwa na majibu bunifu kupatikana kwa changamoto zinazokabili jamii za kikanda na kimataifa” amesema Profesa Nombo.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael Chibunda, amesema mkutano huo umelenga kuunganisha watafiti na wadau kushughulikia changamoto za dunia zinazohusu afya, usalama wa chakula, mazingira na tabianchi.

Profesa Chibunda amesema pamoja na mambo mengine SUA ikiwa ni Taasisi mwenyeji, inajivunia kuwa nguzo ya jukwaa hilo la kubadilishana mitazamo, kuunda ushirikiano na kutafsiri utafiti kuwa vitendo hasa katika sekta ya misitu ambayo imekuwa chachu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho amesema, chuo kimendelea kuongoza katika tafiti za uhifadhi wa misitu, mazingira , wanyamapori, utafiti wa nishati mbadala ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuni, na mbinu za kilimo endelevu zisizo na madhara kwa ardhi na misitu.

“Tunashukuru serikali na wizara kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vyuo vikuu kufanya tafiti ambazo zinakwenda kutoa majibu ya changamoto kisera na kuwagusa wananchi moja kwa moja na katika mkutano huu wa pili wa muungano wa vyuo hivi tunaimani tutapiga hatua kubwa,” amesema Profesa Chibunda.

Profesa Chibunda amewahimiza watafiti na washiriki kushirikiana, kubadilishana mawazo na kuunda mikakati ya kudumu kwa ajili ya jamii zinazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, kwa kufanya majadiliano yenye tija pamoja na matokeo yatakayoacha alama chanya kwa vizazi vijavyo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button