Mwinyi aahidi ajira kwa vijana

PANGAWE, Zanzibar: MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema sera kuu ya Serikali atakayoiongoza katika awamu ijayo itakuwa ni kuimarisha ajira kwa vijana.
Akihutubia mamia ya wananchi katika Uwanja wa Magirisi-Nyarugusu, Jimbo la Pangawe, Dk. Mwinyi amesema Serikali inalifahamu vyema changamoto ya ajira na imejipanga kulitafutia suluhisho la kudumu. Alisema mikakati itahusisha kuendelea kutoa ajira serikalini, kuhamasisha sekta binafsi na kuwawezesha vijana kupata mikopo isiyo na riba kwa ajili ya kujiajiri na kuanzisha biashara.
Aidha, Dk. Mwinyi alibainisha kuwa Serikali imesaini mikataba ya ujenzi wa barabara kuu na za ndani katika Jimbo la Pangawe, pamoja na kujenga shule 29 za ghorofa, ambapo jimbo hilo litapata mgao. Pia alisema kuna mpango wa kujenga viwanja vya kisasa vya michezo kwa lengo la kukuza vipaji vya vijana.
Aliwaomba wananchi kumpa ridhaa ya kuongoza Zanzibar kwa awamu nyingine na kuhakikisha ushindi wa CCM kwa kupiga kura kwa wingi. SOMA: SMZ kuboresha huduma za umeme
Medical debt had me stressed, but this online approach has been a blessing. I now earn about $7,700 monthly. Details >>>> https://dailycash21.blogspot.com/
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com