TRA yavuka lengo kwa kukusanya tril 8.9/-

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh trilioni 8.97 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026.

TRA imeeleza hayo kupitia taarifa yake kwa umma kuhusu makusanyo yaliyopatikana katika robo ya kwanza ya mwaka huo wa fedha, kuanzia Julai hadi Septemba 2025.

Taarifa hiyo imeeleza makusanyo hayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 106.3 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 8.44, ambayo pia ni sawa na ukuaji wa asilimia 15.1, ikilinganishwa na kiasi cha Sh trilioni 7.79 kilichokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2024/2025.

SOMA: TRA makusanyo juu 78% miaka minne

“Makusanyo haya ni sawa na ukuaji wa asilimia 104, ukilinganisha na kiasi cha Sh trilioni 4.40 kilichokusanywa katika kipindi kama hicho toka Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani mwaka wa fedha 2020/2021. Wastani wa makusanyo kwa mwezi pia umeongezeka toka kiasi cha Sh trilioni 1.47 kwa mwezi mwaka 2021/2022, mpaka kufikia Sh trilioni 2.99 kwa mwezi kwa mwaka 2025/2026,” imeeleza taarifa hiyo.

Pia, TRA imesema kwa mara ya kwanza Septemba mwaka huu ilikusanya Sh trilioni 3.47 kwa mwezi mmoja, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko miezi mingine ya nyuma kama hiyo.

Mamlaka hiyo imesema ufanisi huo wa makusanyo umechangizwa na TRA kuendelea kuboresha mahusiano na walipakodi nchini, kuongezeka kwa uwajibikaji wa ulipaji kodi wa hiari, kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi kutokana na sera nzuri za uchumi na mazingira ya biashara yaliyowekwa na serikali.

Imetaja sababu zingine ni matokeo chanya ya uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji biashara nchini kutokana
na kuanzishwa Dawati la Uwezeshaji Biashara na mwitikio wa wafanyabiashara wanaofanya biashara za mtandaoni kwa kampeni za usajili na ulipaji kodi.

TRA imeeleza kuendelea kusimamia utendaji kazi kumewezesha kufikia ufanisi huo.

Taarifa hiyo imeeleza TRA imeendelea kuimarisha usimamizi wa vyanzo vyote vya forodha kupitia matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Forodha (TANCIS) ulioboreshwa.

Imeeleza mamlaka hiyo imeendelea kuhimiza matumizi ya mashine za kielektroniki na kutumia mifumo ya ndani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kubainisha kiasi cha kodi ambacho kila mlipakodi anatakiwa kulipa na kufuatilia kwa karibu.

Taarifa imeeleza TRA imeendeleza kuweka kipaumbele katika utoaji wa huduma bora zinazozingatia mahitaji ya walipakodi, kupitia kuwahudumia walipakodi siku za mapumziko kupitia ofisi zote za TRA.

TRA imeeleza inawezesha biashara kuendelea kufanyika kupitia majadiliano na wafanyabiashara kuendelea kuboresha mahusiano na wafanyabiashara kushirikiana na walipakodi, kuwasikiliza na kutatua changamoto za walipakodi wote nchini, kupitia Programu ya Mabalozi wa Kodi nchini.

Mamlaka hiyo imesema menejimenti yake itaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu usimamizi wa kodi na uhamasishaji wa ulipaji kodi kwa hiari.

Imesema TRA itaendelea kuwezesha ufanyikaji wa biashara nchini kupitia Dawati la Uwezeshaji Biashara na kuendelea kuimarisha usimamizi wa utoaji wa Risiti za Kielektroniki (EFD) nchini.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button