Bil 19.1/- zatumika kujenga vyuo vya VETA 4

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekabidhi vyuo vinne vya Ufundi Stadi na Huduma kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), vilivyopo Njombe, Simiyu, Rukwa na Geita, kwa gharama ya jumla ya shs bilioni 19.13.

SOMA: Bil 100/- kuanzisha ujenzi vyuo vya Veta 62

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo mkoani Njombe, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Frederick Salukele, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu ya ufundi ili kuwawezesha vijana kupata ujuzi utakaowawezesha kuchangia katika uchumi wa nchi.

Vile vile Dk Selukele ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa za mafunzo kupitia VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (FDC) ili kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa VETA, CPA Anthony Kasore, ameshukuru Serikali kwa kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa uwekezaji mkubwa katika miundombinu na vifaa vya kisasa, huku akisema vyuo hivyo vitatoa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya karne ya 21.

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button