Magonjwa ya kinywa yatajwa kuathiri moyo

MAGONJWA ya kinywa kwa watoto, yakiwemo kuoza kwa meno na mafindofindo (Tonsillitis), yameelezwa kuwa yanaweza kusababisha magonjwa ya valvu za moyo endapo hayatatibiwa kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa leo na Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) – Hospitali ya Dar Group, Dk. Aitham Mohamed, wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Tiba Mkoba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayoendelea katika Viwanja vya Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam.
Dk. Aitham amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya matatizo ya meno, kinywa na moyo, akifafanua kuwa kuharibika kwa meno husababisha kuwepo kwa bakteria ambao wanaweza kusambaa mwilini na kushambulia valvu za moyo, hali inayoweza kusababisha magonjwa makubwa ya moyo.
“Tunaihimiza jamii kulinda afya ya kinywa kwa kusafisha meno angalau mara mbili kwa siku. Hatua hii husaidia kuzuia kuoza kwa meno na magonjwa ya kinywa yanayoweza kuhatarisha afya ya moyo,” alisema Dk. Aitham. Ameongeza kuwa wagonjwa wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo hupimwa afya ya kinywa kabla ya upasuaji, ili kuzuia uwezekano wa maambukizi ya bakteria baada ya upasuaji.
Kwa upande wake, Daktari wa Upasuaji wa JKCI -Hospitali ya Dar Group, Dk. Joyce Mkodo, amesema kambi hiyo inalenga kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wenye changamoto mbalimbali za kiafya, zikiwemo vidonda sugu.
“Tunafanya kambi hii kama sehemu ya kusherehekea mafanikio ya miaka 10 ya JKCI katika kutoa huduma za moyo. Tunawahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuchunguza afya zao kabla matatizo hayajawa makubwa,” alisema Dk. Joyce. SOMA: Majaliwa ataka tafiti za tija mabadiliko sekta ya afya
Naye mkazi wa Mbagala, Ibrahim Ndube, amepongeza huduma hizo, akisema zimewasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata matibabu bila gharama kubwa. “Huduma ni bora sana. Nimepata ushauri wa madaktari wa kinywa, mgongo na moyo. Afya ni mtaji wa maisha, hivyo ni muhimu kwa vijana kupima afya mara kwa mara,” alisema Ndube.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com