APC yaongoza kampeni ya usafi na afya Arusha

ARUSHA: CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) kwa kushirikiana na wadau wa afya pamoja na vilabu vya michezo ‘jogging’ mkoani hapa wamefanya usafi na kuhamasisha wananchi kujitokeza kutiki Oktoba 29 mwaka huu ikiwemo maandalizi ya tamasha kubwa la michezo litakalofanyika Oktoba 18 mwaka sanjari na upimaji wa afya bure.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa APC, Cloud Gwandu amesema tamasha hilo linalengo la kupunguza magonjwa yasiyoambukiza ni sanjari na utoapimaji wa afya pamoja na mada mbalimbali zitatolewa kutoka kwa wadau wa sekta ya afya ikiwemo kusisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu

“Kinga kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza ni mazoezi na aina ya vyakula tunavyokula shime tujitokeze siku hiyo lakini mazoezi ni muhimu ili tuwe na afya njema lakini pia wananchi jitokezeni Oktoba 29 kupiga kura ili kuchagua viongozi bora kwa Taifa letu eneo litakapofanyika tamasha hili tutalitangaza hapo badaaye,”amesema.

Amesisitiza michezo ya aina mbalimbali itakuwepo ikiwemo upimaji wa afya pamoja ambapo eneo husika la kufanyia michezo hiyo litatangazwa rasmi muda muafaka ukifika

Wakati huo huo, Dk, Charles Mkombachepa ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesisitiza wananchi ,wanahabari na vilabu vya michezo mkoa wa Arusha kwaajili ya tamasha la michezo ikiwemo kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza ambapo pia wataalam wa afya ya akili watakuwepo ikiwemo huduma za dharura zitakuwepo

Huku Khalid Khasimu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kituo cha Kaloleni akishukuru huduma za afya zilizoboreshwa hivyo pongezi ziende kwa Rais Samia Hassan Suluhu na mmoja kati ya wananchi waliofika kupata huduma za afya kituo cha Kaloleni, Caroline Kingalu akiishukuru serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi na kusisitiza hakuna sababu ya wananchi kutopiga kura sababu huduma katika sekta ya afya zimeboreshwa na wananchi wanapata huduma bora kuanzia kwa mama na mtoto hadi wazee.

Wakati huo huo katika kuelekea katika kilele cha tamasha hilo Oktoba 18 mwaka huu wanachama wa Arusha Jogging Club ,wanahabari na madaktari wamefanya usafi katika vituo viwili vya afya vya Kaloleli na Levolosi kwaajili ya kuhamasisha wananchi mbalimbali kujitokeza kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu nchi nzima

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button