Viongozi wa dini wakumbushwa kupiga kura

MWANZA: VIONGOZI wa dini wa madhehebu ya kikristo mkoani Mwanza wamekumbuswa juu ya umuhimu ya upigaji kura pamoja na kuwakumbusha waumini wa madhehebu yao kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa leo Oktoba 11 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda wakati wa mkutano na viongozi wa madhehebu ya kikristo mkoani Mwanza.
Mtanda amesema Serikali itaendelea kutimiza wajibu na kusimamia Haki kwa kuweza kuhimiza wananchi kupata haki ya kupiga kura kama hitaji la msingi.
“Serikali imetimiza jukumu lake la kuweka mazingira wezeshi ya uchaguzi na viongozi wa wa dini wanatakiwa kuendelea kukumbusha waumini wao kwa muda uliobaki juu ya upigaji kura,”amesema.
Amesema ni vigumu kutenganisha viongozi wa dini na Serikali kwa kuwa viongozi wa dini na Serikali wamekuwa wakifanya kazi za kusaidia wananchi kwa pamoja.
Amesema Kupiga kura sio suala jipya, bali kupiga kura kunasaidia sana katika kuleta maendeleo na maendeleo yatagusa watu wote wenye dini zote.
Mtanda amesema tunapiga kura kwa kuwa tumevuka miaka 18 na tumepata sifa za kupiga kura kwa mujibu wa katiba.
Katika hatua nyingine, Mtanda ametaka makundi mbalimbali ya wafanyabiashara, bodaboda na mama ntilie kutosusia uchaguzi.
Kwa upande wake aliyekuwa Waziri, Lazaro Nyalandu amepongeza viongozi wa dini kwa mchango wao katika kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu.
Amesema viongozi wa dini ni watu muhimu sana katika kusaidia wananchi kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo.
Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ni wakati muhimu wa Watanzania wote kuwa wamoja katika kulinda amani na umoja.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Mwanza,Charles Sekelwa ameomba waumini wa madhehebu yote ya kikristo kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com