Kampeni kufuta taarifa za kizushi iwe endelevu

KATIKA dunia ya sasa yenye kasi kubwa ya teknolojia, mawasiliano yamekuwa rahisi kupitia simu janja, mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijiti.

Hata hivyo, maendeleo haya yamekuja pia na changamoto kubwa ya kuenea kwa taarifa za uzushi, potofu na zisizothibitishwa.

Ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha anaelewa athari za kusambaza taarifa hizo na kuchukua hatua madhubuti kuzizuia.

Kwa mujibu wa sheria za nchi, ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, mtu yeyote anayesambaza taarifa za uongo au zinazoweza kusababisha taharuki, anaingia hatiani kisheria.

SOMA: TCRA waanzisha kampeni ulinzi mitandaoni

Zaidi ya adhabu kisheria, msambazaji wa taarifa hizo anakuwa amechangia kwa namna moja au nyingine katika kuvuruga amani, kuharibu sifa ya taifa na kuwasaidia watu wabaya kueneza hofu miongoni mwa wananchi.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa mstari wa mbele kupitia Kampeni yake ya ‘Futa Delete Kabisa’ katika mapambano dhidi ya utumaji na usambazaji wa taarifa za uongo na zenye taharuki.

Kampeni hiyo yenye zaidi ya miaka 10, inalenga kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kufikiria kabla ya kusambaza taarifa na kuchukua hatua ya kufuta ujumbe usio sahihi.

Mamlaka imekuwa ikitoa elimu kupitia  eedio, televisheni, mitandao ya kijamii na semina.

Tuna imani yapo matokeo, kwa maana ya wananchi kuelewa kuwa usambazaji wa taarifa za uongo au zenye taharuki si jambo dogo, bali ni kosa lenye madhara makubwa kijamii, kitaifa na hata kwao binafsi.

Hata hivyo, katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, imebainika kuwapo watu wanaotumia fursa za kisiasa kueneza uzushi kwa lengo la kuibua hofu.

Usambazaji holela wa taarifa katika kipindi kama hiki unaweza kuathiri amani ya nchi.

Hiki ni kipindi kinachohitaji umakini mkubwa na uwajibikaji wa pamoja kati ya serikali, vyombo vya habari, wadau wa mawasiliano na wananchi kwa ujumla.

Hivyo, tunahimiza elimu kuhusu matumizi salama ya teknolojia haipaswi kukoma. TCRA na wadau mbalimbali hawana budi kuendelea kuelimisha jamii bila kuchoka.

Tunasema hivi kutokana na ukweli kwamba, wapo watu wanaojikuta wakihusishwa na makosa ya mtandao si kwa makusudi, bali kwa kutojua.

Hasa katika enzi hii ya matumizi ya akili unde ambazo taarifa feki zinaweza kutengenezwa kwa urahisi zaidi. Njia pekee ya kuwanusuru wananchi ni kuwapa elimu sahihi, wakafahamu umuhimu wa kutosambaza kila wanachotumiwa wakitambua kwamba katika sheria, hakuna utetezi wa kwamba hawakujua.

Kwa ujumla, ni wajibu wa kila mwananchi kutafakari kabla ya kuamua kutuma ujumbe mahali popote. Kila Mtanzania azingatie kwamba kufuta ni kinga na kusambaza uzushi ni kosa.

Tunaendelea kuunga mkono juhudi za TCRA na wadau wengine katika kuijenga Tanzania salama, yenye mawasiliano yenye tija na heshima katika dunia ya sasa ya kidijiti, tukihimiza kampeni ya kufuta taarifa za uongo na uzushi iwe endelevu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button