Bagia kutoka Iringa zinaweza kuwatoa akina mama kimasomaso- Ngajilo

IRINGA: Wajasiriamali wadogo, hasa akina mama, wana fursa kubwa ya kujikwamua kiuchumi kupitia utengenezaji wa bagia—kitafunwa rahisi kinachopendwa na watu wa rika zote nchini.
Kwa ubunifu na mipango mizuri ya masoko, bidhaa hii ya kawaida inaweza kugeuka kuwa biashara yenye faida kubwa, ikiwa chanzo cha ajira na mapato kwa familia nyingi.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni kata ya Mkwawa, mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia CCM, Fadhili Ngajilo, alisema ni wakati sasa akina mama wakatumia ubunifu wao katika ujasiriamali ili kuinua kipato, badala ya kutegemea misaada.
Alisema akina mama wakijipanga vizuri, wanaweza kutengeneza bagia bora, kuzihifadhi kwenye vifungashio vya kuvutia, na kuziuza kwenye masoko makubwa kama Dodoma na Dar es Salaam, ambako mahitaji ni makubwa kutokana na wingi wa watu.
“Elimu ya ujasiriamali itatolewa kila mahali, na nitawasaidia muyafikie masoko hayo ya Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya vitafunwa,” alisema Ngajilo.
Kama ilivyo Dar es Salaam alisema, Dodoma ina watu wengi, wanafunzi wa vyuo vikuu, wafanyakazi na wageni wengi jambo linalofanya soko la bidhaa hiyo liwe kubwa.
“Ukisafirisha bagia zako kutoka Iringa saa 11 alfajiri, saa mbili asubuhi zinafika Dodoma—hapo unaweza kuuza bagia zako zikiwa bado na harufu ya yake!”
Ngajilo alisema wajasiriamali wengi wanashindwa si kwa kukosa bidhaa, bali kwa kutokuwa na mtazamo wa kibiashara.
Akitolea mfano wa baadhi ya matajiri nchini alisema wengi walianzia kwenye vitu vidogo. Kuna waliouza barafu, chapati, pipi, au keki—leo ni mamilionea.
“Unachodharau ndicho kinaweza kukutoa kimaisha. Ukichelewa, Wajanja kutoka nje wataiona fursa hii na kuifanya yao, wataziuza kila mahali. Kabla hawajatuibia teknolojia, tuanze sisi,” alisema.
Ngajilo pia aliahidi kuimarisha miundombinu ya masoko, kuunganisha wajasiriamali na taasisi za mikopo ya riba nafuu, na kuhakikisha elimu ya biashara inawafikia wananchi wote.
Aidha Ngajilo alisisitiza umuhimu wa kulinda heshima ya jina la Mkwawa akisema:
“Kata hii ya Mkwawa imebeba jina la chifu anayejulikana duniani. Tunatakiwa kufanya mambo yatakayomuendeleza kihistori hata kutengeneza sanamu yake. Mimi ni mtu kazi, nitafanya kazi na wananchi kuibadilisha Mkwawa iwe ya kisasa.”
Google pays $220 an hour online. My close relative had been unemployed for nine months, but last month, she received a $25k paycheck by working from home for 10 hours a day. Everyone should try this job now—just use this link.
COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com