Askofu ataka watanzania kuhubiri amami

ARUSHA: ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya International Evangelism Church(IEC) Tanzania, Askofu Eliudi Isangya amewataka watanzania kila mmoja kwa imani yake kuhubiri amani ili uchaguzi ufanyike kwa amani bila machafuko na wale wenye nia ovu na nchi wapuuzwe kwani sio mila na destuli ya mtanzania walizoachiwa na waasisi wa nchi hii.
Askofu Isangya amesema hayo leo katika ibada maalumu iliyoandaliwa na IEC ya kuliombea taifa amani na kuhamashisha watanzania kushiriki kupiga kura katika uchaguzi utaofanyika Oktoba 29 mwaka huu katika ibada iliyofanyika Makao Makuu ya IEC Sakila wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na maskofu, wachungaji na waumini wa kanisa hilo mkoani Arusha ibada iliyohudhuriwa na mamia ya watu.
Amesema baadhi ya nchi za nje haiitakii mema Tanzania kwa kuwa amani na utulivu na kufanya chaguzi kwa utulivu na amani na kufuata misingi ya demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa na hali hiyo inaziumiza nchi nyingi na kuamua kupandikiza chuki kwa watanzania ila aliwaomba watanzania kuwapuuza wachochezi na kila mmoja kw aimani yake atenge muda wa kuliombea Taifa baada ya mambo haya ya pamoja na kuiiombe nchi ya Tanzania.
Askofu Isangya alisema kuna baadhi ya watu wanahubiri machafuko na kuna watu wanahamashisha maandamano ili watu wasipige kura watu hao hawatafanikiwa kwa kuwa Mungu yuko nyuma ya watanzania wenye kuiombea amani na mipango yao kwa kutala nchi iingie katika machafuko kamwe hawatafanikiwa kwa kuwa watanzania ni waelewa.
Alisema leo wako hapo zaidi ya watu 1000 wakiombea nchi amani na kushiriki kupiga kura ili waweze kumchagua Rais,Mbunge na Diwani na makanisa ya IEC yaliyopo katika Mikoa yote nchi na nje yanaliombea Taifa na wenye kuitakia mabaya Tanzania wapuuzwe kwani wanataka watoto wasiende shule.akina mama na vijana wasifanye biashara na wakulima wasilime ama kuvuna mazao yao kwa hila zao kwani hilo kamwe haliwezekani.
“Naamini Rais Rais Samia Suluhu Hassan atachaguliwa na watanzania kwa kuwa nchi inaongozwa kwa kufuata misingi yademokrasia sambamba na upigaji kura wea kuchagua na kuchaguliwa na hilo litatimia mwishoni mwa mwezi huu kwa kila mmoja kushiriki kupiga kura” alisema.
Askofu Issangya Naye mchungaji Eunice Sumari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa IEC Tanzania alisema makanisa ya IEC yalifanya ibada kama hiyo mwezi agosti mwaka huu na ibada hiyo maalumu ya mwezi octoba ni ya pili hivyo ana uhakika kuwa yale mabaya yanatengenezwa na watu wanaotumiwa na mataifa ya nchi hayatafanikiwa kwa kuwa Mungu ameyapokea maombi ya waumini wa makanisa hayo na uchaguzi utafanyika kwa amani na Rais Samia Suluhu Hassan atachaguliwa kwa kura nyingi kama Mwenyezi Mungu alivyompangia kwa kuwa ana nia njema na nchi kwa kuiletea maendeleo.
Alisema nchi isiyokuwa na amani wanaotesekana ni akina mama na watoto kwani ndio walezi wakubwa wa familia hivyo yeye kama mwenyekiti wa akina mama wa IEC kamwe hawezi kukubali amani ya nchi ivunje kwa maslahi ya wachache atakuwa mstari w ambele kuliombea taifa.
Naye Mchungaji Julius Kimaro ambaye ni mwalimu alisema Tanzania ilipata uhuru kwa amani kwa kuwekwa misingi iliyoachwa na wasisi wa hivyo kufanyika kwa maombi ni kuwakumbusha waumini na kuwaelimisha waumini kumrudia Mungu na kuilinda amani kama vitabu vya dini vinavyosema wachache waliomba na walifanikiwa kwa ajili ya wenye nia ofu ya nchi yao.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com