UWT:Wapuuzeni wanaopiga kelele,mkapige kura

KATIBU MKUU wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Susan Kunambi, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, na kutozingatia kelele za wale wanaotaka kuharibu amani ya nchi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba, Angellah Kairuki, Kunambi alisema kelele hizo ni jaribio la kuwatia hofu wananchi, lakini amesisitiza kuwa hali ya usalama itabakia nzuri. “Msiwe na hofu tarehe 29. Tutoke tukatiki kuchagua CCM, na amani ya Tanzania itadumu. Kelele za wale wanaokuambia msitoke ni za kudhoofisha tu, msizisikilize,” alisema Kunambi.

Ameongeza kuwa wale wanaosema “No reforms, No election” wanapojaribu kuwatia hofu wananchi, wanapita vibaya kwa sababu CCM ina kaulimbiu yenye matokeo chanya. Aidha, Kunambi alimuombea kura mgombea ubunge, Angellah Kairuki, akisema kuwa ni kiongozi hodari, mchapakazi na mtu wa wananchi. “Hamtajuta mkiwa na shida. Sio kwamba hamtamuona, mtakuwa naye kwenye shida na raha. Tumemchagua mtu sahihi, mkampe kibali tarehe 29,” alisema Kunambi. SOMA: CCM yaahidi kukabili wanyama waharibifu

Aidha, Kunambi alimuombea kura Mgombea Urais, Dk Samia Suluhu Hassan, akisema kuwa amefanikisha miradi mikubwa ya maendeleo nchini, ikiwemo maji mitaani, zahanati, shule, Bwawa la Mwalimu Nyerere, treni ya kisasa, daraja la Magufuli, na kuhamisha serikali Dodoma. Alihakikisha kuwa Dk Samia ni mkweli, mvumilivu na anayesimamia amani, utulivu na umoja wa nchi. “Hatafanya kazi peke yake; mchague na madiwani wa CCM na leo Msigani tunaye Zaidi Muliro, wakili mkamchague akabuni miradi manispaa,” alisema Kunambi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button