CCM yaahidi kukabili wanyama waharibifu

MOROGORO: MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema kuwa endapo CCM itapewa ridhaa ya kuongoza tena serikali katika kipindi cha miaka mitano ijayo, itaweka mkazo mkubwa katika kukabili wanyama waharibifu wanaovamia mashamba kwa kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani, ili kulinda mazao na kuongeza tija kwa wakulima.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kilombero juzi jioni, Dk Nchimbi alisema tayari serikali imeshaanza maandalizi ya mfumo huo utakaotumika kuwafukuza tembo na wanyama wengine waharibifu, kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika ili kuhakikisha mazao ya wananchi yanabaki salama wakati wote wa uzalishaji.

“Nataka niwahakikishie nitashiriki kuhakikisha mipango ya kutumia ‘drones’ kuwafukuza wanyama waharibifu inatekelezwa. Hii itawasaidia wakulima wetu kuendelea kuzalisha bila hofu, mazao yaongezeke na nchi yetu iendelee kupata maendeleo,” alisema.

Aidha, alibainisha kuwa katika sekta ya kilimo, Serikali ya CCM imepanga kuimarisha zaidi uzalishaji kwa kuanzisha mashamba darasa yatakayowapa mafunzo wakulima kuhusu kilimo cha mazao yenye tija kubwa kama michikichi, ufuta, parachichi na korosho.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button