Upasuaji: Binti aondolewa uvimbe wa kilo 7 Kagera

KAGERA: Jopo la madaktari wa upasuaji likishirikiana na wataalamu mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera limefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa kwa binti mwenye umri wa miaka 14 na kumuondolea uvimbe mkubwa uliokuwa kwenye via vyake vya uzazi, uliokuwa na uzito wa kilo saba.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali hiyo, Dk. Emmanuel Absalum Mwakasumi, amesema binti huyo alifikishwa hospitalini akisumbuliwa na maumivu makali ya tumbo, tatizo la kutopata choo mara kwa mara, pamoja na hali ya kujihisi kushiba muda wote hata bila kula chakula.
“Baada ya kufanya vipimo, tuligundua kuwa ana uvimbe mkubwa kwenye via vya uzazi upande wa kushoto. Tuliamua kufanya upasuaji, na tunamshukuru Mungu umefanikiwa kwa mafanikio makubwa bila changamoto yoyote. Uvimbe huo ulikuwa na uzito wa kilo saba, na kama asingefika hospitalini mapema, angeweza kupata madhara makubwa zaidi,” alisema Dk Mwakasumi.
Ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa uliotolewa na wataalamu wa kada mbalimbali waliokuwa sehemu ya timu hiyo ya upasuaji.
Dk Mwakasumi alifafanua kuwa aina hiyo ya uvimbe inaweza kujitokeza tangu mtu anapozaliwa, kutokana na seli maalumu zinazohusika katika ukuaji wa mwili wakati mwingine kuhama kutoka eneo lake la asili na kukua sehemu isiyotakiwa, jambo linaloweza kusababisha uvimbe au matatizo mengine ya kiafya.
Ametoa wito kwa wazazi na wananchi kwa ujumla kufuatilia afya zao na kuchukua hatua mapema wanapohisi mabadiliko yoyote yasiyo ya kawaida katika miili yao.
“Kuna wananchi wengi wamekuwa wakisubiri hali iwe mbaya zaidi ndipo waende hospitalini. Hili si jambo jema, kwani kuchelewa kupata matibabu kunasababisha matatizo makubwa ya kiafya ambayo yangedhibitiwa mapema,” aliongeza Dk Mwakasumi.
Real and simple method for all to use and do some surfing over internet and start making more than $17k every single month from home. i have made and received recently $16829 from this job and i do only 1 or 2 hours a day on my mobile. yeah its that much simple even work onl mobile in your part time. get this right now and start making income from home just by follow instructions here.
More Details For Us→→ http://www.job40.media
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $27,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….>>> https://www.Homeprofit1.site