NMB,Itilima waboresha utoaji mikopo ya asilimia 10

SIMIYU: Benki ya NMB kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, imeendelea kutekeleza mfumo mpya wa utolewaji mikopo ya halmashauri asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu katika halmashauri hiyo.
Ikiwa ni awamu ya pili benki hiyo kuwezesha kutoa mikopo hiyo ndani ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mfumo huo ambao ni jumuishi, jumla ya Sh milioni 156.6 zimetolewa kwa vikundi 19 kutoka katika kata 13 za halmashauri ya wilaya hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kutolewa kwa mikopo hiyo Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri, Jonathan Buluba alisema kuwa walipokea maombi kutoka katika vikundi 36.
Alisema kuwa vikundi hivyo viliomba mkopo wenye thamani ya Sh milioni 661.06, ambapo baada ya uhakiki kupitia kamati mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB vilibaki vikundi 19.
“Uhakiki huu ulikuwa unafanyika wazi, vikundi hivyo vilihakikiwa na kamati ya mikopo ngazi ya kata, halmashauri, kamati ya uhakiki ngazi ya wilaya kisha Benki ya NMB, na leo vimepatikana vikundi 19 kati ya 36 ambavyo viliomba,” alisema Buluba.
Alisema kuwa vikundi vya wanawake vilivyopata ni 10 vikipatiwa mkopo wenye thamani ya Sh milioni 78, vijana vikundi 6 mkopo wa Sh milioni 62.5 na vikundi vya watu wenye ulemavu vitatu vikipata mkopo wa thamani ya Sh milioni 16.1.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano Mwandamizi Biashara za Serikali kutoka NMB, Irene Masaki alisema kuwa mbali na vikundi hivyo kupatiwa mikopo, wamepewa mafunzo ya jinsi ya kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Alisema kuwa NMB itaendelea kuwapa elimu wanufaika wa mikopo hiyo pamoja na kuwasimamia katika biashara zao, ili kuwawezesha kufanya marejesho kwa usahihi pamoja na kutumia fedha hizo katika malengo kusudiwa.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com