Landlover Festival kuibua fursa za utalii Iringa

Mkoa wa Iringa unajiandaa kupokea mafuriko ya watalii, wafanyabiashara na wadau wa michezo ya magari kupitia Landlover Festival 2025, tamasha kubwa litakalofanyika kuanzia Novemba 28 hadi 30 mwaka huu.

Akizungumza katika maandalizi ya tamasha hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wadau wa Utalii Iringa, Serafino Lanzi, alisema wadau wa utalii wameipokea kwa mikono miwili hafla hiyo kwa imani kwamba itakuwa na mchango mkubwa katika kutangaza utalii wa ndani na kuongeza mwamko wa wananchi kutembelea vivutio.

“Kama wadau wa utalii, jukumu letu ni kutangaza utalii wa ndani. Tumeipokea Landlover Festival kwa sababu inaunganisha utalii, michezo na biashara. Iringa itakuwa kitovu cha matukio hayo,” alisema Lanzi.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Landlover Festival, Augustino Namfua, alifafanua kuwa lengo kuu la tamasha hilo si kusherehekea kuyaona magari ya aina hiyo, bali pia kukuza utalii katika maeneo yenye vivutio vinavyojulikana na visivyojulikana.

“Msafara wa magari utaelekea kwenye vivutio mbalimbali vilivyoko Iringa. Hii itasababisha shughuli za utalii kusisimka, wajasiriamali kupata fursa za biashara na wageni wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania kufika,” alisema Namfua.

Namfua aliongeza kuwa zaidi ya magari 500 yanatarajiwa kushiriki tamasha hilo, likiwa na washiriki zaidi ya watu 1,000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Afisa Utalii Kanda ya Kusini, Sixtus Malangalila, alisema;
“Tunafurahia kuona Iringa ikiongoza juhudi za kufungua Kusini kiutalii. Landlover Festival si tukio la kawaida litajenga mtandao wa biashara na utalii katika mikoa ya nyanda za juu kusini.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, alisema maandalizi ya mapokezi ya wageni yanaendelea, na maeneo maalum yametengwa kwa ajili ya shughuli hizo.

“Wageni watapokelewa River Valley Campsite na Kihesa Kilolo, ambako msafara mkubwa wa magari aina ya Landlover utaanzia kuelekea Uwanja wa Samora,” alisema Sitta.

Ameongeza kuwa kilele cha tamasha hilo kitakuwa tarehe 30 Novemba, ambapo msafara wa magari utaelekea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, moja ya vivutio vikubwa zaidi barani Afrika, ikiwa ni sehemu ya kukuza utalii na kuutangaza mkoa wa Iringa.

“Iringa ina vivutio zaidi ya 34. Tamasha hili ni jukwaa la kuyatangaza, kuibua fursa za kibiashara na kuimarisha uchumi wa wananchi,” alisisitiza Sitta.

Mbali na burudani na matembezi ya magari, washiriki wa Landlover Festival watashiriki pia katika shughuli za kijamii kwa kusaidia jamii zenye uhitaji, hatua ambayo inalifanya tamasha hili kuwa lenye kugusa jamii moja kwa moja.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button