Mabasi mwendokasi kufika Buza, Chamazi, Kigamboni

WAZIRI wa Ujenzi, Abdalla Ulega amesema mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ana mkakati wa kupanua mradi wa mabasi yaendayo haraka ndani ya Wilaya ya Temeke. Ulega alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Samia katika Viwanja vya Tanesco Buza wilayani Temeke jana na akabainisha mkakati huo unahusisha kufikisha mabasi ya mwendokasi Buza, Chamazi na Kigamboni.

“Watu wa Mbagala ni mashahidi, miaka minne iliyopita walikuwa wakiingia katika madirisha, huku wakilazimika kulipa nauli mara mbili kwa kugeuza na gari ili tu waweze kupata siti. Lakini tangu Rais Samia aingie madarakani, sasa wanapanda kwa raha zao. Hakuna kugombania, ndani ya kiyoyozi,” alisema. SOMA: Latra yatangaza nauli mpya mwendo kasi, teksi

Ulega alisema serikali imeongeza bajeti ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Dar es Salaam hadi kufika Sh trilioni 1.7 zilizowezesha jiji hilo kuwa na barabara za mwendokasi. Aidha, alisema serikali imeongeza bajeti ya Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kutoka Sh bilioni 300 hadi Sh bilioni 600 zilizowezesha kujenga barabara kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 226 ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button