INEC yatoa maagizo matano upigaji kura

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeagiza wapigakura waliopoteza kadi waruhusiwe kupiga kura kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), hati ya kusafi ria au leseni ya udereva.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhani ilieleza kuwa, kama taarifa za mpigakura zipo katika daftari lililopo kwenye kituo husika lakini amepoteza kadi yake au kadi yake imeharibika, ataruhusiwa kupiga kura.

Kailima alisema wapigakura hao wataruhisiwa ikiwa tu majina yake yaliyopo katika kitambulisho atakachowasilisha yatafanana na majina yote yaliyomo kwenye daftari la wapigakura.

Ilieleza kuwa, kwa mpiga kura ambaye picha yake haipo kwenye daftari la kudumu la wapigakura lakini ana kadi ya mpiga kura yenye taarifa binafsi zilizomo katika daftari hilo pia ataruhusiwa kupiga kura.

INEC ilisema kwa wapigakura ambao namba ya kadi yake ya mpiga kura inatofautiana namba ya mpigakura iliyomo katika daftari la kudumu la wapigakura lakini picha na majina ya kwenye daftari hilo ni sawa, ataruhusiwa kupiga kura. SOMA: INEC yaonya wanaojiandikisha mara mbili daftari la wapiga kura

Pia, wapigakura wote kutoka katika kata 10 zilizofuatwa na wapigakura wake kuhamishwa katika kata za jirani lakini kadi zao zinaendelea kusoma taarifa za awali za vituo vyao vya zamani vilivyofutwa. Ilizitaja kata hizo kuwa ni Kata ya Kanoge, Litapunga, Katumba, Mtapenda, Kijiji cha Ikolongo na Ndurumo na Jimbo la Nsimbo Kata ya Mishamo, Ilangu, Bulamata na Ipwaga zilizopo katika Jimbo la Tanganyika.

Nyingine ni Kata ya Milambo, Igombemkulu na Kanindo zilizopo katika Jimbo la Ulyankulu Wilaya ya Kaliua. Kadhalika, INEC ilisema kuwa haitamruhusu mpigakura yeyote ambaye ana kadi ya kupigia kura lakini taarifa zake hazipo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ https://dailycash21.blogspot.com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button