INEC yaonya wanaojiandikisha mara mbili daftari la wapiga kura

TUME ya Huru ya  Taifa ya Uchaguzi (INEC)  imewatoa rai kwa wananchi kutojiandikisha zaidi ya mara moja katika Daftari  la Kudumu la Wapiga Kura  litakaloanza katika Desemba 11 -17 mwaka huu  kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dodoma .

Aidha uboreshaji wa daftari hilo kwa mwaka 2924/25 utatumia teknolojia ya BVR Kits zilizoboreshwa kwa kuwekewa programu endeshi ya kisasa zaidi zilizo rahisi kubebeka na kufanya zoezi hilo kuwa rahisi haswa maeneo ya vijijini

Mweyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC), Jaji Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema hayo wakati wa mkutano kati ya NEC na wadau wa uchaguzi mkoani Arusha wakiwemo viongozi wa dini, wawakikishi wa asasi za kiraia, wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari, makundi mbalimbimbali ya vijana na watu wenye ulemavu, wanawake na wazee wa kimila.

Advertisement

Jaji Mwambegele amesema  kujiandikisha zaidi ya mara moja  ni kosa la kisheria kwakuzingatia masharti ya kifungu  Cha 114(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais ,Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 kinachoeleza mtu yoyote atakayeomba kuhakikisha zaidi ya mara moja atakuwa ametenda kosa la kisheria na akitiwa hatiani adhabu yake ni faini isiyopungua kiasi  cha sh,100,000 na isiyozidi sh,300,000 ama kutumikia kifungo Kwa kipindi kisichopungua miezi sita na kisichozodi miaka miwili gerezani au vyote.

“Wananchi kujiandikisha zaidi ya mara mbili ni kosa hivyo nawaomba viongozi mliohidhuria hapa  mkawaelimishe wananchi wasijiandikishe zaidi ya mara moja ili kupeuka ivunjaji wa sheria”

Amesema kwa sasa tume hiyo inafanya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kuanzia Desemba 11 hadi 17 mwaka huu katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dodoma ikiwemo halmashauri za Wilaya ya Kuondoa, Chemba na Mji wa Kondoa ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia  saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni