Takukuru yapania kudhibiti rushwa, ubadhirifu

KIGOMA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa magari matatu waliyokabidhiwa na serikali yataiwezesha taasisi hiyo katika kuongeza mapambano dhidi ya rushwa na usimamizi wa miradi unaozingatia viwango na taratibu.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Kigoma, Asha Kwariko alisema hayo akipokea magari matatu aina ya ‘Toyota Land Cruiser Hard Top’ ambayo taasisi hiyo imekabidhiwa kwa ajili ya watendaji wa taasisi hiyo katika wilaya za mkoa Kigoma.

Mkuu huyo alisema kuwa vitendea kazi hivyo vitawawezesha kufika kwa wananchi maeneo ya pembezoni ya mkoa kwa ajili ya kutoa elimu, kukabiliana na matukio ya rushwa lakini pia kutembelea na kukagea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa Kigoma.

Alisema kuwa magari hayo ambayo yametolewa kwa wilaya za Uvinza, Kakonko na ofisi ya TAKUKURU mkoa ambapo magari hayo yanafanya mkoa huo kuwa na magari sita ambayo yatawezesha watendaji kuzungumza maeneo yote ya mkoa kwa uhakika.

Akizungumza wakati akizindua na kukabidhi magari hayo, Mkuu wa mkoa Kigoma, Balozi Sirro ameitaka taasisi hiyo kuyatumia magari hayo kutekeleza majukumu yao kikamilifu, kuwa waadilifu, uzalendo na kuwafikia wananchi kwa haraka sambamba na kutumia magari hayo kwa majukumu yaliyokusudiwa ili kuwafanya wananchi kuwa na Imani na utendaji wa taasisi hiyo.

Sambamba na hilo Balozi Sirro amewataka wananchi kutoa taarifa na ushahidi dhidi ya vitendo vya rushwa lakini ubadhirifu kwenye miradi bila kumuonea mtu na kutoa taarifa sahihi ambazo zitasaidia taasisi hiyo katika kuzifuatilia na kuzifanyika kazi taarifa zinazotolewa.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button