TMA yashukuru uwekezaji wa Dk. Samia

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Kanda ya Magharibi imepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya mamlaka hiyo, hatua iliyowezesha kufanikisha utabiri sahihi wa hali ya hewa kwa zaidi ya asilimia 91.7.
Meneja wa TMA Kanda ya Magharibi, Waziri Waziri, alisema uwekezaji huo umeimarisha uwezo wa mamlaka hiyo kufanya tathmini na kutoa utabiri sahihi wa hali ya hewa, hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kwa wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Aidha, Bw. Waziri alisema kwa msimu wa mvua wa mwaka 2025/2026, maeneo mengi ya Kanda ya Magharibi yanatarajiwa kupata mvua za kiwango cha chini hadi cha wastani, zenye mtawanyiko usioridhisha, huku kukitarajiwa ongezeko dogo la mvua kuanzia mwezi Februari hadi Aprili 2026. SOMA: Hali ya hewa yaonya ongezeko la mvua



