Swala dume na uwezo kumiliki majike 100

TANZANIA ni nchi iliyobarikiwa kuwa na aina nyingi za vivutio vya utalii vikiwamo vya wanyamapori kama swala wa aina mbalimbali wanaopatikana katika mapori ya akiba na hifadhi nyingi za taifa.
Miongoni mwa aina mbalimbali za swala hao ni pamoja na sitatunga (nzohe) puku, swalapala nyumbu, pofu, kudu, kuro, tohe, swala granti na taya. Uwepo wa wanyama hawa ni faida kubwa kwani baadhi hupatikana Tanzania pekee. Hao ni pamoja na swala aina ya sitatunga (nzohe).
Kimsingi, wanyamapori hao na aina nyingine wanapaswa kulindwa dhidi ya ujangili ili wasipotee kwani huonekana kwa urahisi katika kipindi utalii na kuwa kivutio na chanzo kikubwa cha mapato nchini. Swala ni mnyamapori anayepatikana maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Afrika na Asia.
Kwa mujibu wa chapisho la Mtandao wa Wildlife Tanzania, duniani kuna aina 90 za jamii ya swala. Katika Bara la Afrika pekee, zipo jamii 71. Kutokana na kuwa na aina nyingi ya jamii za swala, watu wengi wanashindwa kutofautisha majina yao kutokana na mfanano wao katika mwonekano.
Hata hivyo, wanyamapori hao wana tofauti kubwa kimaumbo, rangi, tabia na namna wanavyoishi. Licha ya mfanano wao, majina ya kisayansi ya wanyama hao yamekuwa tofauti kwa sababu wametawanyika katika maeneo mbalimbali duniani.
SOMA: Serengeti hifadhi bora Afrika kwa mara ya tano
Kutoka na mtawanyiko huo, baadhi ya majina ya swala yametokana na tabia au sehemu wanazopatikana katika mabara mbalimbali duniani. Inaelezwa kuwa, wanyamapori hao wana sifa mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine, zinasababisha kuwapo aina za swala duniani.
Kutokana na kutawanyika kwa wanyamapori hao katika maeneo mbalimbali duniani, Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa wa wanyamapori hao katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba. Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro ni kati ya hifadhi yenye idadi kubwa ya swala hawa.
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori, Kamhanda Mateso ambaye pia ni mwongoza watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi anaeleza aina tofauti za familia za swala.
Anasema wapo swala wadogo, swala wadogo na swala wa kubwa ambao ni wakubwa kuliko wote. Swala wanaishi katika makundi au ngome inayoongozwa na dume. Dume mmoja anaweza kuwa na majike kuanzia 40 hadi zaidi ya 100 na ili kuongoza kundi, madume ni lazima wapigane na mshindi ndio ataongoza kundi.
“Kwenye familia moja hata akizaliwa swala dume pamoja na jike, dume moja litamiliki majike yote yatakayokuwepo ndani ya familia hiyo,” anafahamisha. Kwa mujibu wa Mateso, licha ya dume moja kumiliki majike mengi, pia swala jike nalo linakuwa na madume wengi.
Sifa nyingine ana uwezo wa kushi bila kunywa maji kwa muda mrefu endapo anakula nyasi zenye ubichi. “Swala ana uwezo wa kuishi kwa kula hizo nyasi na kupata maji ya kutosha na hana haja ya kwenda kutafuta maji sehemu nyingine,” anasema Mateso na kuongeza kuwa, wanyamapori hao wana uwezo mkubwa wa kunusa na kuona hali inayowasaidia kujilinda dhidi ya adui zao.
Swala huwasiliana kwa njia ya sauti inayotolewa kama ishara mmojawapo anapoona au kubaini kuwapo adui au hatari. Kwa mujibu wa mateso, wanyamapori hao wana manyoya laini na mazito yenye rangi nzuri inayowasaidia kujificha dhidi ya maadui.
Anasema ngozi za wanyama hao huwasaidia kujikinga na dhidi ya mionzi ya jua kali au baridi kutokana na kuwa na mafuta mengi. Mwongoza watalii huyo anasema pembe za wanyama hao zina mikuno inayosadia wakati wa kujitoa ngozi na kuwatofautisha baina ya jamii moja na nyingine.
Anasema swala ana mtindo wa kuruka juu kwa miguu yote kwa wakati mmoja anapokimbia na hii huonesha tahadhari, nguvu au afya kwa mnyama kuwa, ana uwezo wa kukimbia zaidi kuliko adui yake. Anasema swala wana chenga nyingi wanapokimbia hali inayowasaidia kwa kufanya ugumu adui zao kama simba, duma na fisi kuwakamata.
Wanyama hao wana uwezo mzuri wa kuruka juu japo hawawezi kupanda miti kutokana na umbile la miguu yao yaani kuwa na kwato. Pembe za wanyama hao hujitoa ngozi kila mwaka ili kukua vizuri na kufanya wawe na mwonekano tofauti kutoka aina moja na nyingine.
Anasema muda wa kuishi swala unaweza kuchukua miaka kama 15 na baada ya hapo hukuchukuliwa na kupelekwa kwenye hifadhi ndogo na huko wana uwezo wa kuishi hadi miaka 24. Kuhusu swala wenye manyoya mengi na ya kuvutia aina ya kuro, Mateso anasema wanapatikana maeneo ya wazi, nyasi au miti mirefu pia kando ya sehemu zenye maji maji.
Kupatikana kwao kwenye maeneo hayo huwasaidia pia kujikinga dhidi ya maadui zao. Kwa mfano, ukienda kwenye hifadhi nyingi za taifa, swala ni rahisi kumuona kuliko wanyama wengine wakubwa. Aina nyingine za swala ni pamoja na impala anayejulikana kwa kuruka kwake kwa nguvu na kwa kasi.
Kwa mujibu wa wanasayansi, swala aina ya impala ni miongoni mwa wanyama wanaovutia zaidi. Maisha ya impala porini ni takribani miaka 12 hadi 20. Ni mnyama mwenye shughuli za saa 24. Wanasayansi na wahifadhi wa wanyamapori wanasema swala wengi jamii ya impala huishi maisha ya pamoja na wana aina tatu za vikundi ambayo ni majike, watoto na madume.
Mimba ya swala hudumu kati ya miezi sita na nusu hadi saba yaani kati ya siku 194 hadi 200) na kisha mtoto mmoja huzaliwa. Ni nadra sana kwa wanyamapori hawa kuzaa pacha yaani watoto zaidi ya mmoja kutokana na ujauzito mmoja.
Usiku wa kuzaa, majike huondoka kwenye kundi na hurudi baada ya wiki chache tangu kuzaa kwake wakati mwanae ndogo akikua na kupata nguvu zaidi.
Kwa upande wa kuro ambao ni jamiii ya swala wenye manyoya mengi na ya kuvutia, Mateso anasema wanapatikana maeneo ya wazi, nyasi au miti mirefu pia kando ya sehemu zenye majimaji. Kupatikana kwao kwenye maeneo hayo huwasaidia pia kujikinga dhidi ya maadui.
Kwa mfano, katika hifadhi nyingi za taifa ni rahisi kumuona kuliko wanyama wengine wakubwa. Hivyo uwepo wa wanyama hawa nchini Tanzania ni faida kubwa kwani ni chanzo cha mapato kutokana na shughuli za utalii wa ndani na nje.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com