Wajumbe wateule waapishwa

ZANZIBAR : SPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Zuberi Ali Maulid, amewaapisha wajumbe wateule wa Baraza hilo leo, kufuatia uteuzi uliofanywa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Taarifa ya uteuzi huo ilitangazwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said, ikibainisha kuwa wajumbe hao wameapishwa rasmi kuanza majukumu yao katika Baraza la Wawakilishi. SOMA:  Dk. Mwinyi awateua wajumbe wapya

Wajumbe  hao walioapishwa ni Sharif Ali Sharif, Masoud Ali Mohammed, Dk. Saada Mkuya Salum na Nadir Abdullatif Alwardy. Wengine ni Idrisa Kitwana Mustafa, Tawfik Salim Turky, Said Ali Juma na Dk. Juma Malik Akil.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button