Ligi ya vijana Arumeru kuendelea kesho

ARUSHA: Mashindano ya Ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13 yanatarajiwa kuendelea kesho Novemba 8 kwa michezo minne itakayochezwa katika viwanja vya Shule ya Kimataifa Kennedy House, Usa River Wilaya ya Arumeru.

Jumla ya timu 8 zinashiriki ligi hiyo iliyoandaliwa na kituo cha kukuza soka kwa vijana cha ‘Young Boys Academy’ kilichopo Arumeru mkoani Arusha.

Michezo minne itachezwa ambapo mechi ya kwanza  itazikutanisha timu za Satino Academy dhidi ya timu ya Follow Your Dream Academy mchezo utakaoanza saa nne asubuhi.

Ligi ya vijana yashika kasi Arumeru

Arusha Young Stars itacheza  dhidi ya Arusha Youth Academy, Mirrior Academy itaikaribisha Peace youth Academy na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Young Boys Academy dhidi ya Chuga Boys.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Young Boys imejikusanyia pointi 28, ikifuatiwa na Satino Academy yenye pointi 22 nafasi ya tatu Mirrior Academy yenye point17 , nafasi ya nne Arusha Youth pointi 17.

Kwa mujibu wa waandaaji ,mashindano hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwasaidia vijana kuweza kukua katika vipaji  vyao vya mpira.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. They supply me $80 5 an hour to finish art work on an Apple laptop. I surely didn’t think it became possible, but my depended on friend made $26,000 in simplest four weeks working on this clean opportunity and she or he or he endorsed me to give it a try. Discover more instructions through manner of manner of

    visiting the next link=====➤ https://Www.Smartpay1.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button