Polisi yaanika athari vurugu uchaguzi, yasaka wanane
JESHI la Polisi nchini limebainisha athari kubwa zilizotokana na vurugu, uporaji na uvunjifu wa amani vilivyotokea Oktoba 29, mwaka huu katika maeneo mbalimbali nchini.
Pia, limesema linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watu 10, akiwemo Askofu Josephat Gwajima na viongozi waandamizi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime vurugu zilizojitokeza katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Shinyanga, Geita, Songwe, Ruvuma, Mara, Dodoma, Kilimanjaro na Iringa zilisababisha athari kubwa ikiwemo vifo vya watu, uharibifu na uchomaji moto wa mali za umma na binafsi.
“Matukio hayo yalisababisha kupotea kwa maisha ya watu, kuchomwa moto mali za serikali na za binafsi, ikiwemo Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mahakama, ATM za benki na baadhi ya vituo vya polisi,” alisema Misime.
Aidha, alieleza kuwa vituo vya mabasi ya mwendokasi kuanzia Kimara Mwisho hadi Magomeni na kutoka Magomeni hadi Morocco vilivamiwa na kuharibiwa, huku baadhi ya barabara za lami na zege zikichomwa moto kwa kutumia matairi. Majengo kadhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia yaliharibiwa kwa moto.
Misime alisema mali binafsi hazikuachwa, kwani maduka, vituo vya mafuta, magari makubwa na madogo na pesa za wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali ziliibwa na kuharibiwa.
“Pamoja na kwamba baadhi ya waliopanga na kutekeleza uhalifu huo wamekamatwa na kuanza kufikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta wale wote waliopanga, kuratibu na kutekeleza uovu huo,” alisema.
Alibainisha watu 10 wanatafutwa kwa ajili ya kukamatwa na kuhojiwa kuhusiana na matukio hayo, akiwemo Askofu Josephat Gwajima, Brenda Rupia, John Mnyika, Godbless Lema, Machumu Kadutu, Deogratius Mahinyila, Boniface Jacob, Hilda Newton, Award Kalonga na Aman Golugwa.
Hata hivyo, tayari Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata Aman Golugwa ambapo wakili wake, Hekima Mwasipu alithibitisha kuwa alikamatwa jana asubuhi akiwa nyumbani kwake, ingawa hakueleza eneo halisi la kukamatwa kwake.
Kwa mujibu wa Mwasipu, hadi kufikia jana mchana walikuwa bado wakifuatilia kujua Golugwa amechukuliwa na kupelekwa kituo gani. Pia, alithibitisha kuwa mtu mwingine aliyekamatwa ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Boniface Jacob maarufu ‘Boni Yai’, aliyekamatwa maeneo ya Goba, Dar es Salaam.
Misime aliongeza kuwa uchunguzi wa kina unaendelea na kwamba hatua stahiki tayari zimeanza kuchukuliwa dhidi ya wahalifu waliokwishakamatwa ambapo baadhi yao walifikishwa mahakamani Novemba 7, 2025.
Aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa sahihi zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wote wa vurugu hizo, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au kikundi chochote kitakachopanga au kutekeleza uhalifu.
“Jeshi la Polisi linaonya kuwa mtu au kikundi cha watu wanaopanga kufanya uhalifu wa namna yoyote ile, halitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi yao,” alisisitiza Misime.
Wakati huohuo Shirikisho la Waendesha Bodaboda na Bajaji Dar es Salaam limetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao pamoja na kuharibiwa mali zao katika vurugu zilizotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, mwaka huu na kuhimiza amani.
Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Saidi Kagomba alieleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akisisitiza wanaunga mkono tamko la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila la kuwataka madereva hao kutambuliwa rasmi kwa mfumo maalumu.
Alisema tayari utekelezaji wa agizo hilo umeanza na zaidi ya madereva 17,000 wameshasajiliwa hadi sasa katika mfumo huo maalumu, alitoa mwito kwa Watanzania kuendelea kulinda amani ya nchi, kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani, na kuchukua tukio hilo kama fundisho.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
1. Josephat Gwajima
2. Brenda Jonas Rupia
3. John Mnyika
4. Godbless Jonathan Lema
5. Machumu Maximillian Kadutu
6. Deogratius Cosmas Mahinyila
7. Boniface Jacob
8. Hilda Newton
9. Award Kalonga
10. Amaan Golugwa
https://youtu.be/GSMZ_7h0GHE?si=Zpiu_1OUDfZr6KLo
1. Josephat Gwajima
2. Brenda Jonas Rupia
3. John Mnyika
4. Godbless Jonathan Lema
5. Machumu Maximillian Kadutu
6. Deogratius Cosmas Mahinyila
7. Boniface Jacob
8. Hilda Newton
9. Award Kalonga
10. Amaan Golugwa
https://youtu.be/VP3Pn8f_u-c?si=0lP1ji42vd_c7gug
1. Josephat Gwajima
2. Brenda Jonas Rupia
3. John Mnyika
4. Godbless Jonathan Lema
5. Machumu Maximillian Kadutu
6. Deogratius Cosmas Mahinyila
7. Boniface Jacob
8. Hilda Newton
9. Award Kalonga
10. Amaan Golugwa
https://youtu.be/yW1q7jaJooY?si=cNs6ifK2nNAUD_th
Police name 10 people wanted over nationwide riots as crackdown intensifies across Tanzania
1. Josephat Gwajima
2. Brenda Jonas Rupia
3. John Mnyika
4. Godbless Jonathan Lema
5. Machumu Maximillian Kadutu
6. Deogratius Cosmas Mahinyila
7. Boniface Jacob
8. Hilda Newton
9. Award Kalonga
10. Amaan Golugwa
https://youtu.be/yW1q7jaJooY?si=cNs6ifK2nNAUD_th