Yanga inakong’ota tu

DAR ES SALAAM; YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo Uwanja wa KMC, Kinondoni, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa an Maxi Nzengeli, Andy Boyeli aliyefunga mawili na Pacome Zouzoua, wakati la KMC lilifungwa na Daruweshi Saliboko.

Kutokana na ushindi huo Yanga imefikisha pointi 10 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, ikishinda michezo mitatu na kutoka sare mmoja.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button