Asia Halamga ashinda ubunge Hanang

Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) imemtangaza Asia Halamga kuwa mshindi wa nafasi ya ubunge jimbo la Hanang kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Hanang mkoani Manyara, Geogrey Abayo alisema kuwa Asia Halamga alipata kura 173,330 sawa na asilimia 99.3.

Akitangaza matokeo katika kituo cha majumuisho ya kura ya Rais na mbunge ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Oktoba 30, 2025 alibainisha kwamba wananchi waliojiandikisha kupiga kura ni 196,630,waliopiga kura ni 174,449 ambapo kura halali ni 173,343,
kura zilizokataliwa ni 1,106.
Aidha, mbunge Asia Halamga kama mgombea pekee alikabidhiwa hati ya ushindi na hati ya kuchaguliwa rasmi kuwa Mbunge wa Jimbo la Hanang.
Kwa upande wake, Mbunge Asia alipongeza INEC kwa kuratibu zoezi la uchaguzi ambalo limetoa fursa kwa wananchi kujitokeza kupiga kura mapema na kuendelea na shughuli kutokana na uwepo wa vituo vingi vya kupigia kura.
Alisema wananchi wa Hanang wanachohitaji ni kutimiza ajenda ya maendeleo pekee kwa kudumisha amani ambayo ndio msingi wa maendeleo hayo.



