Wazazi wasipuuze jitihada elimu ya lishe kwa watoto

WAZAZI inawapasa wajitahidi kuwapatia watoto makundi ya vyakula, angalau yanayopatikana kwa urahisi kwenye maeneo yao ili kuweza kuwaepusha na utapiamlo.
Pia, mzazi anapokuwa anauguza mtoto mwenye utapiamlo, hulazimika kukaa hospitalini na kujigharimia hadi muda ambao mtoto anapata kupona, huku shughuli zake za kiuchumi zikisimama. Licha ya changamoto hizo zinazowakumba watoto wanaopatwa na ugonjwa wa utapiamlo, serikali nayo imekuwa ikigharimia kwa kipindi ambacho mtoto anakuwa wodini kwa wastani wa siku 21.
Pia, naipongeza serikali kwa kutoa Sh bilioni 48.56 kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano aliyekusudiwa Fedha hizo zimekwishatolewa na kutumika kutoa huduma katika afua za lishe, ikiwa ni utengaji huo wa fedha kwa kila halmashauri ambao umeimarika kufikia wastani wa kitaifa wa Sh 1,546.
Wazazi wasipuuze elimu wanayoipata kuhusu suala la makundi ya vyakula vya kuwapatia watoto wao ili kuepusha kupoteza muda wa kusimamia majukumu mengine na serikali kutumia fedha nyingi kutibu ugonjwa huo kwa mtoto. Kusiwepo mzaha katika kuwasikiliza wataalamu wa lishe pindi watoto wanapopelekwa kliniki kwa hatua za awali ambapo masomo kuhusu lishe yanatolewa.
Vilevile, watoto wanapobainika kuwa na uzito uliopungua, wazazi wachukue hatua. Kwa mujibu wa Ofisa Lishe wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, Shinyanga, Mohamed Mkoko katika robo ya mwaka wa pili ya mwaka 2025, wamepokea watoto 22 wenye utapiamlo na watoto 11 walitoroshwa na wazazi wao. Sababu iliyobainika ni wazazi kushindwa kujihudumia hospitalini wakati
Kwa mujibu wa Ofisa Lishe wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, Shinyanga, Mohamed Mkoko katika robo ya mwaka wa pili ya mwaka 2025, wamepokea watoto 22 wenye utapiamlo na watoto 11 walitoroshwa na wazazi wao. Sababu iliyobainika ni wazazi kushindwa kujihudumia hospitalini wakati watoto wakihudumiwa na serikali.
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa ripoti yake mwezi Septemba mwaka 2025 likieleza kwamba watu milioni 43 duniani hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa yasiyoambukizwa, ikiwemo utapiamlo. SOMA: Handeni Mji yaweka mikakati kuimarisha afua za lishe
Kuna kila sababu ya kuipongeza serikali kwa jitihada walizochukua za kuhakikisha ugonjwa wa utapiamlo kwa watoto kuanzia umri wa 0 hadi miaka mitano unakomeshwa, kwani watoto wanapata virutubisho kwa kutumia njia zozote zilizowekwa na wazazi kuendelea kupatiwa elimu. Hivyo, watoto 7,454,996 wenye umri chini ya miaka mitano nchini wamepimwa hali zao za lishe na wengine wamepatiwa matibabu ya utapiamlo mkali. Wazazi na walezi wamepatiwa elimu na unasihi wa lishe na kuhimizwa kuboresha taratibu za uzalishaji wa vyakula kwa watoto ili kupunguza udumavu.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, jumla ya mashine 230 za kunyunyuzia virutubishi kwenye vyakula zimefungwa katika mikoa yote 26 nchini na hivyo kufikia mashine 1,402, ikilinganishwa na mashine 1,172 zilizokuwepo mwaka 2024.
Wizara ya Afya kupitia Taasisi ya Lishe imetekeleza na kuratibu mafunzo kuhusu sayansi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa maofisa 281 yaliyolenga kuwajengea uwezo katika kusimamia na kuratibu Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJTMMMAM) ili kuifikia jamii na kuondoa changamoto zilizopo.
Wazazi hawana budi kuthamini juhudi zilizofanywa na serikali kuhakikisha watoto wote hawapati utapiamlo, kwani wanachotakiwa ni kufuata utaratibu wa ulaji ulio sahihi na bora unaozingatia afya kwa mtoto.



