Wananchi wahimizwa kuchangia damu

WANANCHI mkoani Dodoma wamehimizwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wale wanaopata dharura ya kuhitaji huduma ya kuongezewa damu.

Mkuu wa Timu za Ukusanyaji Damu Kanda ya Kati, Dk Leah Kitundya ametoa hamasa hiyo katika kliniki ya upimaji wa bure wa magonjwa yasiyoambukiza inayoendelea katika bustani ya mapumziko ya Nyerere jijini Dodoma. SOMA: Watakiwa kuchangia damu Muhimbili

Dk Leah alisema kila mwananchi ana wajibu wa kuchangia damu kwa sababu inasaidia wakati wa uhitaji. “Wananhttps://habarileo.co.tz/watakiwa-kuchangia-damu-muhimbili/chi mliopo hapa viwanja vya Nyerere tunawaomba na kuwakumbusha kuchangia damu kwa sababu itatusaidia sote wakati wa uhitaji. Damu yako inaweza kumsaidia mtu ambae hukutegemea ingemfikia.

Amewaita wananchi kuchangia damu huku akiwakumbusha kujitokeza kwa wingi kujitolea kwa sababu zinapotokea ajali ama dharura za kuhitaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha wapo pia ndugu na jamaa wa karibu wanaweza kukumbwa na kadhia hiyo.

Balozi wa Taasisi ya Magonjwa Yasiyoambukiza (NCD), Lawrence Malima ambae pia ni msanii wa Bongo fleva aliungana na wataalamu wanaotoa elimu kuwasisitiza wananchi kutengeneza utamaduni wa kupima afya ili kugundua maradhi yanayowasumbua huku akichombeza na nyimbo za hamasa.

“Kliniki hii ni muhimu kwa sababu itawasaidia kufahamu ni magonjwa gani yanawasibu. Lakini hata wale ambao tayari wanaugua watapata huduma za awali hapa na watajua hali zao zinaendeleaje,” alisema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button