Samia: Wizara maalum ya vijana kuanzishwa

DODOMA: RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali ya awamu ya sita imejipanga kabisa kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana kupitia uundaji wa wizara maalumu itakayoshughulikia masuala ya vijana pamoja na washauri maalumu.

Akifungua Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Kwanza nchini Dodoma, Rais Samia amesema wizara hiyo itawezesha kupanua fursa za kiuchumi kwa vijana na kuimarisha mchango wao katika maendeleo ya taifa. SOMA: Waliofata mkumbo kwenye maandamano waachiwe

Katika hotuba yake, Rais Samia alisema serikali katika kipindi hiki cha pili imedhamiria kutumia kikamilifu mikakati ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, na kuibua mpango mpana wa utekelezaji wa Dira 2050.  “Tutazingatia zaidi sekta muhimu za uzalishaji ikiwemo utalii, viwanda na madini ili kuongeza ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 5.6 hadi asilimia 7 na kuimarisha masoko ya mitaji.”

Dira 2050 inaweka dira ya muda mrefu ya taifa la Tanzania kuwa “taifa lenye uchumi thabiti, wa ushindani, jumuishi na wa ustawi wa kila mwananchi”. Mpango huo umejikita kwenye nguzo tatu kuu ikiwemo Uchumi imara, jumuishi na ushindani, Uwezo wa binadamu na maendeleo ya kijamii pamoja na  Utamaduni, mazingira na maendeleo endelevu.

Serikali pia imetoa kipaumbele cha kiwango cha rasilimali kwa vijana kwa kutenga Sh bilioni 200 kwa ajili ya mikakati ya siku 100 za awali, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwaongeza vijana kwenye masuala ya maendeleo na fursa za ajira. Aidha, wizara maalumu itakayoundwa itachukua jukumu la kusimamia na kuratibu sera za vijana, ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo ya ushauri, mafunzo na uwekezaji.

Akihitimisha, Rais Samia aliwataka viongozi wa serikali, wabunge na wadau wa maendeleo kuhakikisha utekelezaji wa mikakati ya Dira 2050 unachukua sura ya vitendo, na si tu kauli. “Sekta binafsi ni nguzo muhimu ya kukuza uchumi serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa ajili ya wote,” alimalizia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button