Serikali kuongeza ukuaji kilimo hadi 10%

SERIKALI katika miaka mitano ijayo, inakusudia kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta za uzalishaji, ikianza kilimo lengo llikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta hiyo kutoka asilimia 4 ya sasa hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

Dhana itakayoongoza mpango huo ni “Kilimo ni Biashara, Mkulima ni Mwekezaji”.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati akifungua na kuhutubia Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Novemba 14, 2025, bungeni mkoani Dodoma.

SOMA: Rais Samia afungua Bunge 13

Amesema kwa kufanya hivyo, serikali inalenga sio tu kujihakikishia utoshelevu wa chakula, bali pia kuwekeza kwenye mnyororo wa thamani ili kuwanufaisha Watanzania wengi walioajiriwa kwenye sekta hiyo ili  kusudi likiwa kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya mahindi, mchele na mbogamboga (Horticulture), barani Africa.

“Tutafanya hivyo kwa kujielekeza kwenye kilimo cha kisasa kwa kuongeza pembejeo kama mbegu bora, mbolea na viuatilifu kwa ruzuku, tutaongeza upatikanaji wa maji ya uhakika na kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka ekari milioni 3.4 hadi ekari milioni 5, kwa kukamilisha ujenzi wa mabwawa na skimu za umwagiliaji zinazoendelea na kuanzisha skimu mpya ikiwemo kwenye bonde la Mto Rufiji,” amesisitiza Rais Samia.

 

Aidha, amesema serikali itaanzisha vituo vya ukodishaji zana za kilimo, ambavyo vitatoa huduma za matumizi ya teknolojia katika kilimo chetu.

Samia amesema ili kukuza uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo, benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya Ushirika zitaimarishwa ili zichochee mapinduzi yayoyatazamia.

Mkuu huyo wa nchi amesema: “Pamoja na kuongeza uzalishaji, lazima pia tudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno (post harvest loss). Hivyo, tutaendelea kuwekeza katika kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao chini ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).”

Amesema serikali itazidi kuboresha mifumo ya stakabadhi ghalani ambayo imeshaanza kuwaletea manufaa wakulima wa mazao mbalimbali yaliyojumuishwa kwenye mfumo huo.

Katika kupanua masoko ya nje, na kutumia fursa za diplomasia ya uchumi kuyatumia masoko ambayo tayari nchi imefushafungua, serikali itahakikisha kuwa fursa hizo zinakuwa na makubaliano yanayotekelezeka ili kuwa na uhakika wa masoko hayo.

Rais Samia amesema katika hilo masoko yanayokusudiwa ni ya mbaazi, choroko na ufuta, kupata masoko ya uhakika.

Pamoja na kujitosheleza kwa chakula kwa 128% kwa sasa, mwelekeo ni kuendelea kupiga hatua kwenye uzalishaji wa sukari na mafuta ya kupikia hususan uzalishaji na usindikaji wa alizeti, chikichi na ufuta.

Amesema kwa mazao ya biashara ambayo yalikuwa yakifanya vizuri na kuwanufaisha wakulima wengi, lakini yameathiriwa na ama bei za soko duniani, au wawekezaji waliopewa viwanda vya kuchakata mazao hayo kushindwa kuviendesha vyema viwandahivyo yatasimamiwa kwa karibu zaidi ambayo ni Chai, Kahawa, Parachichi na Pamba shabaha ikiwa kupanua masoko, kuongeza ushindani wa bei na kuwafaidishazaidi wakulima wa Tanzania.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. Cash generating easy and fast method to work part time and earn an extra $15,000 or even more than this online. By working in my spare time I made $17990 in my previous month and I am very happy now because of this job. you can try this now by following
    the details here…… https://Www.Smartpay1.site

  2. Cash generating easy and fast method to work part time and earn an extra $15,000 or even more than this online. By working in my spare time I made $17990 in my previous month and I am very happy now because of this job. you can try this now by following
    the details here…… https://Www.Smartpay1.site

  3. Every month, I’m making $19,000+ just by doing Online work at home. Last month, I successfully earned $19,613 and the payment was deposited directly into my bank account. This Online opportunity is remarkable and provides a steady stream of income. It’s easy enough for anyone, even beginners, to start making money Online. Visit this website to begin earning today.

    HERE………….. https://Www.Workapp1.Com

  4. I am making over $25,000 a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life. This is what I do. For more information visit below this website…….

    HERE…………… https://Www.Workapp1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button