Liverpool yamtafakari Olise kuwa mbadala wa Salah

TETESI za usajili zinadai klabu ya Liverpool inamtafakari nyota wa Bayern Munich, Michael Olise (23), kama mbadala wa Mohamed Salah wa Misri (33), na ipo tayari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa.(Fichajes in Spanish)

Arsenal imeingia katika mbio kumsajili Karim Adeyemi, (23) wa Borussia Dortmund huku Manchester United pia ikiwa na nia kupata saini ya mshambuliaji huyo wa Ujerumani. (Teamtalk)

AZ Alkmaar itamruhusu kiungo wa kidachi mwenye umri wa miaka 19, Kees Smit kuondoka lakini inataka ziada ya pauni milioni 22 huku Newcastle, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich zote zikiwa na nia kumsajili. (Sky Sports)

Miamba ya Ufaransa, Paris St-Germain ina nia kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Vinicius Jr kwa uhamisho huru mwaka 2027, wakati mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 na timu ya Real Madrid utakapomalzika. (Fichajes – in Spanish)

Mshambuliaji wa Arsenal na Brazil, Gabriel Jesus, 28, ameeleza shauku yake kurejea katika klabu yake ya zamani, Palmeiras katika siku zijazo. (Mirror)

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button