Wadau wa utalii wahamasishwa kuwania tuzo za Serengeti

WADAU wa uhifadhi na utalii katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamehamasishwa kushiriki katika tuzo za uhifadhi na utalii za Serengeti (Serengeti Awards 2025) zinazotarajiwa kufanyika Desemba, 2025.

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Dainess Kunzugala amesema hayo katika kikao na wadau hao wakiwemo makampuni na waendeshaji wa shughuli za utalii, waongoza watalii, watoa huduma za malazi, wahifadhi na mashirika au taasisi zenye mchango katika uhifadhi kilichofanyika mkoani Iringa.

“Natoa hamasa kwa wadau wetu wa utalii kutumia fursa hii muhimu kutuma maombi yao kuwania tuzo hizi muhimu ambapo kuna kategoria zipatazo saba ambazo zimeainisha makundi mbalimbali” amesema Kunzugala.

Amesema lengo ni kutambua mchango wa wadau hao pamoja na kuifanya sekta ya utalii iwe na mwamko katika kuleta maendeleo nchini.

Naye, Mwongoza Watalii kutoka kampuni ya Mukuta Travel and Tours, Fadhili Laizer ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa elimu ya namna ya kujisajili na kuwania tuzo hizo.

“Wadau wa utalii nyanda za juu kusini na maeneo mengine niwaambie tu ni vyema wakajitokeza kwa wingi kushirikiana kuwania tuzo hizo ili kukuza utalii lakini pia kujitangaza zaidi” amesema Fadhili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Iringa Tourism Association, Serafina Lanz ameishauri Serikali kufikiria kuendeleza mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo ina hifadhi kubwa kama Nyerere , Ruaha na kupendekeza tuzo zijazo ziitwe majina kama Nyerere Awards au Ruaha Awards.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button