‘Milango uwekezaji nishati safi ipo wazi’

NAIBU Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe amesema milango ya uwekezaji wa nishati safi ya kupikia ipo wazi kwa wadau wanaotaka kuwekeza.

Amesema hayo ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake na wadau mbalimbali wa masuala ya hifadhi ya mazingira pembezoni mwa Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaofanyika katika Jiji la Belem, Brazil.

SOMA: Mkakati nishati safi ya kupikia wapata mafanikio makubwa

Prof. Msoffe akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Burn Manufacturing, Caroline Amollo ambayo inajihusisha na utengenezaji wa majiko ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania amemshukuru na kupongeza kwa shughuli hizo.

Amemuleza mdau huyo kuwa Serikali ya Tanzania inatambua jitihada za wadau wa maendeleo kama kama hao katika kuchangia upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu kwa wananchi kote nchini.

“Sote tunapaswa kutambua kuwa nishati safi si tu gesi kama ambavyo watu wengi wanafikiri lakini ni njia yoyote ile ambayo unaweza kuitumia katika kuivisha chakula ili mradi usiharibu mazingira kwa kukata miti ovyo,” amesema.

Kwa upande wake, Caroline ameshukuru Serikali kwa kutambua mchango wadau hususan wanaounga mkono juhudi za kukabiliana na changamoto za mazingira kutokana na ukataji wa miti.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website

    More Details For Us→→  http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button