Maopareta Jeshi la Magereza waaswa weledi

MKUU wa Jeshi la Magereza Tanzania CGP Jeremiah Yoram Katungu, ametoa wito kwa Maafisa na askari wataalam wa simu za upepo, kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na kuhakikisha wanatunza siri za ofisi wakati wote wa kutekeleza majukumu yao.

CGP Katungu ameyasema hayo leo Novemba 20, 2025 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo maopareta wa simu za upepo wa jeshi hilo nchi nzima Msalato jijini Dodoma.

Amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalam hao wa jeshi ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi ikiwemo usahihi wa taarifa, kujua umuhimu wa utunzaji wa siri za ofisi na kuwa na nidhamu.

SOMA: Magereza washauri malezi bora watoto wa kiume

Amewataka washiriki wa mafunzo hayo wapatao 239, kuwa makini wakati wote wa mafunzo na kutumia vizuri mijadala itakayoendeshwa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Aidha CGP. Katungu amesema Jeshi la Magereza lilianza kutumia simu za upepo Mwaka 1959 katika Gereza la Ukonga la jijini Dar es salaam, likiwa na redio sita, akieleza hatua iliyopigwa na jeshi ambapo kwasasa zaidi ya vituo 137 vimeshafungwa redio hizo ambazo zimetajwa kurahisisha mawasiliano ndani na nje ya jeshi.

Katika hatua nyingine CGP. Katungu ameishukuru serikali kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutengwa kwa bajeti kwa ajili ya masuala ya mawasiliano, vyombo vya usafiri na mitambo ya kilimo, hatua inayosaidia kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Akitoa neno la utangulizi, Kamishna wa Utawala na Rasilimaliwatu Jeshi la Magereza, CP Ahmad Mwen-dadi, amemshukuru CGP Katungu kwa kuridhia kufanyika kwa mafunzo mbalimbali ndani ya jeshi, ikiwemo ya maopareta wa simu za upepo akieleza kuwa, yameleta manufaa makubwa kwa Maafisa na Askari katika kuboresha utendaji wa kazi zao.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button