Omolo Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Dk Mapana Naibu

DAR ES SALAAM; RAIS Dk Samia Suluhu Hassan amemteua Jenifa Omolo kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi  Dk Moses Kusiluka, iliyonukuliwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu,  imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Omolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia ameteua Dk Kedmon Mapana kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana. Kabla ya uteuzi huo Dk. Mapana alikuwa Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button