Rais Mwinyi awateua makatibu wakuu

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu wapya wa Wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Said  imesema kuwa Fatma Mabrouk Khamis ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Teknolojia ya Habari na Ubunifu,Khamis Suleiman Mwalimu   ameteuliwa kuwa KatibuMkuu  Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Dk habiba  Hassan Omar ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya  Biashara na Maendeleo ya Viwanda.

Wengine walioteuliwa ni  Dk Rahma Salim Mahfoudh kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango , Salama Mbarouk Khatib yeye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji .

Rais Mwinyi  pia amemteua Mattar Zahor Masoud  kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Saleh Mohammed  Juma atakuwa  Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo , Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Mhandisi Ali said  Bakari akipangiwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. SOMA: Omolo Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Dk Mapana Naibu

Katika uteuzi huu umeambatana sambamba na uteuzi wa manaibu makatibu wakuu ambapo Rashid Ali Salum ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Makame Machano Haji akiwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari , Sanaa , Utamaduni na Michezo.

Wengine Khalid Masoud Waziri  akipangiwa  Wizata ya Vijana, Ajira  na Uwezeshaji na Mohammed Dhamir  Kombo akipelekwa Wizara ya kilimo , Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo na Amosi John Hennock akienda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Hatahivyo katika uteuzi huo Rais Dk Mwinyi  ameamua kuwaacha  Makatibu Wakuu kumi na mbili katika Wizara zao kadhalika na Manaibu Makatibu  kumi ambao nao wataendelea katika wizara zao za awali .Wateule  wote wanatarajia kuapishwa rasmi siku ya Jumamosi wiki hii  22 Novemba  katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button