Dk Kijaji ataka utu maliasili, utalii

MOROGORO: WAZIRI mpya wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji na naibu wake Hamad Chande, wamewataka maofisa na askari wa uhifadhi nchini kuendeleza utu katika kuwahudumia wananchi, kuendeleza uhifadhi na kuwakinga wananch dhidi ya wanyama wakali na waharibifu na kuwakirimu wageni katika utalii.

“Leo tumefika hapa Tawa (Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania), nawapongeza sana na tumekabidhi magari manne, pikipiki 33, bajaji na vitendea kazi kama ndege nyuki (drones), hii yote ni kuonesha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuendeleza uhifadhi.

“Msisitizo wetu mimi na viongozi wenzangu wa wizara hii ni kwamba Tawa ni moja ya taasisi inayohudumia watu moja kwa moja kule chini. Nawaagiza katika kazi zenu kuanzia kuendeleza uhifadhi, kuwakinga wananchi dhidi ya wanyama wakali na kupokea watalii muendeleze utu na ukarimu,” alisema Dk Ashatu.

Naye, Naibu Waziri Chande aliwapongeza wahifadhi hao kwa kazi nzuri nchi nzima na kusema viongozi hao wapya wako tayari kushirikiana nao kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Hassan Abbasi, aliyewaongoza watumishi wengine kuwapokea viongozi katika ziara yao ya kwanza kwenye taasisi za uhifadhi tangu walipoteuliwa na kuapishwa, amesema pamoja na kuajiriwa wafanyakazi wengi katika miaka hii minne hii kuliko wakati wowote katika sekta hizo, kazi kubwa pia ya wizara hiyo ni kuendeleza ulinzi wa raslimali wanyama.

“Waziri pamoja na raslimali watu iliyoongezeka sana katika sekta hii, nataka nikujulishe tu utasimamia pia uhifadhi wa raslimali wanyama wakiwemo simba 17,000; nyati 225,000; tembo 60,000 na chui 24,000 walioko nchi nzima kutaja kwa uchache.”

Viongozi hao wanaendelea na ziara za kujitambulisha katika taasisi mbalimbali za sekta hiyo na kukagua miradi ya utalii inayoendelea kutekelezwa.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button