Niffer, wenzake wafikishwa mahakamani

DAR ES SALAAM; MFANYABIASHARA Jeniffer Jovin ‘Niffer’(26)na wenzake 21 wanaokabiliwa na kesi ya uhaini wamefikishwa mahakamani mchana huu kwa ajili ya kesi yao kutajwa.
Niffer na wenzake kesi yao inatajwa leo Novemba 25,2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Lucianus Luchius (28), Paul Malima (28), Augustino Mulwale (30), Mohamed Kondo (30), John Mmena (26), Paul Shirima (23), Ramadhani Ramadhani (21), Levi Mkute (40), Esau Ernest Maarufu ‘Duduye’ (21), Leonard Mkonyi.
Pia wapo Fadhili Nyombi, Hamisi Hamisi, Abeid Kivuyo (24), Nicholous Shiduo (27),Abati Mwadini (27) Mika Chavala (32), Fatuma Mzengo (30), Dewji Ramji (19), Ruthmelda Silaa (21), Hilda Ngulu(22) na Yusuph Hussein(22).
Washitakiwa wanakabiliwa na makosa matatu mbkele ya mahakama hiyo la kwanza likiwa la kupanga njama na mengine mawili ni ya uhaini.



