Dk. Kijaji aagiza ukarabati wa Hoteli Mikumi

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amefanya ukaguzi wa ukarabati mkubwa unaoendelea katika Hoteli ya Mikumi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, hatua inayolenga kuongeza viwango vya huduma za utalii na ushindani wa hifadhi katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Hoteli hiyo, inayomilikiwa na mwekezaji Gullam Abbasi, inafanyiwa ukarabati wa kisasa unaojumuisha uboreshaji wa vyumba, maeneo ya burudani, huduma za kimataifa, na sehemu maalum kwa watoto.Dk. Kijaji amesema uwekezaji huu ni mfano wa ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi unaosaidia kukuza utalii, kuongeza ajira na mapato ya hifadhi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kushirikiana na wawekezaji binafsi kuongeza uwezo wa malazi ndani ya hifadhi zake, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, muda wa kukaa hifadhini, na mapato ya uhifadhi. Hoteli ya Mikumi inatarajiwa kuwa ya kwanza ndani ya hifadhi kutoa huduma za kiwango cha kimataifa, ikiwa na vyumba 46, bwawa la kuogelea, ukumbi wa mazoezi, sauna na maeneo ya burudani kwa watoto. SOMA: Waziri Kijaji aitaka Tanapa kuongeza ubunifu

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button