Mwigulu anusa hujuma vurugu Oktoba 29
WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amesema vurugu siku na baada ya Uchaguzi Mku wa Oktoba 29, mwaka huu zililenga kuhujumu uchumi wa Tanzania.
Dk Mwigulu alisema hayo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam.
Alisema haiingii akilini kuona waratibu wa vurugu hizo si raia wa Tanzania na wanaratibu vurugu hizo wakati wakiwa nje ya nchi.
Dk Mwigulu alisema kigezo kingine kinachoonesha malengo ya walioratibu vurugu wanalenga kuirudisha nchi nyuma kiuchumi ni aina ya maeneo yaliyoshambuliwa.
SOMA: Mwigulu aapishwa kuwa Waziri Mkuu
Alisema kushambulia njia kuu za uchumi ikiwemo miundombinu ya usafiri wa umma, kuchoma vituo vya mafuta na kuchoma kituo cha kupoza umeme ni ishara kuwa lengo ni kuhujumu uchumi.
Aidha, Dk Mwigulu alisema waratibu wa fujo hizo zilizosababisha hasara kwa taifa wanafanya hivyo kwa maslahi yao kwa kuwa wameahidiwa kulipwa fedha ikiwa wakifanikisha kuhujumu uchumi wa nchi na kuirudisha nyuma.
Alisema kubomoa na kuharibu miundombinu zikiwemo ofisi za serikali, kuchoma magari ya serikali na kuchoma vituo vya mafuta ni uhujumu wa uchumi wa nchi.
Dk Mwigulu alisema wakati wa vurugu hizo kulikuwa na madhara ikiwa ni pamoja na kuharibiwa ofisi za serikali zaidi ya 756 na vituo vya mabasi yaendayo haraka 27.
Kadhalika, Dk Mwigulu alisema vurugu hizo zilisababisha kuchomwa moto mabasi ya abiria kwenda mikoa sita na nyumba binafsi 273 huku vituo vya polisi 159 vikiteketezwa.
Alisema katika vurugu hizo zilizotokea siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, vituo binafsi vya mafuta 672 viliharibiwa.
Dk Mwigulu alifafanua kuwa vurugu hizo pia ziliharibu magari ya watu binafsi ambapo zaidi ya magari 1,642 yaliharibiwa pamoja na pikipiki 2,268 huku magari ya serikali yakiwemo ya wagonjwa zaidi ya 972 yakiharibiwa.
“Huu ni uhujumu wa uchumi, Watanzania hawa wote hawa awe na duka au gari lake wanajikusanya sana kufanya haya mambo, hawajanunua magari kwa ziada wanajinyima ili kufanikisha, hayo ndio maisha ya Mtanzania,” alisema Dk Mwigulu.
Alisema kitendo cha vijana hao ambao inasemekana walilipwa fedha ili kutekeleza uovu huo, walitaka kwenda kuchoma moto Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani cha Magufuli pamoja na Kituo cha kuzalisha na kupoza umeme cha Kinyerezi ni ushahidi kuwa ni hujuma na haihusiani na uchaguzi.
“Kuchoma reli si siasa hata kidogo, Watanzania mali hii ni yenu na nchi hii ni yenu inakasirisha zaidi pale unaposikia kuwa wanaofanya hivi wanatumia Kiswahili ili waonekane kuwa ni Watanzania lakini hawapo Tanzania,” aliongeza Dk Mwigulu.
“Na ukitaka kujua kuwa kilichofanywa ni hujuma za kiuchumi, ni kwamba huku kwingine kumetafutiwa sababu, lakini wanafika mbali na kutaka watalii wasiende Tanzania watalii si mali ya serikali bali wana faida hata kwa wananchi wa kawaida, fedha inayopatikana inasaidia kusomesha watoto wa Kitanzania,” alisema.
Dk Mwigulu alihoji kuwa kama si uhujumu wa uchumi, kwa nini mambo haya yanatokea wakati nchi imeboresha bandari zake, imejenga reli ya kisasa ya tano kwa urefu duniani na ya kwanza Afrika huku idadi ya watalii ikipaa?
“Hawa wanaowajenga vijana kufanya haya na kuwalipa, wana maslahi na Tanzania na watazirejeshaje fedha hizo na Watanzania amkeni wale wenzenu wapo nje na familia zao, wakiwachochea nyie mkiuana wao ndio wanafurahi zaidi,” aliongeza.
Alisema jambo hilo ni hujuma ya waziwazi dhidi ya taifa na kuwataka Watanzania waamke na kuwashtukia
watu hao kwani wanafanya hayo wakati mradi wa makaa ya mawe umeanza na mradi wa chuma cha Liganga na
gesi asilia vimeanza kuinufaisha nchi.
Dk Mwigulu aliwataka Watanzania kukataa kuchochewa kuichoma nchi yao kwani mambo hayo huwa yanatokea pale nchi inapoanza kufaidika na rasilimali zake kwani wananchi wakiwa pamoja watu hao wanashindwa kupora rasilimali za taifa.
Aliweka wazi kuwa Tanzania ni ya Watanzania na italindwa kwa gharama yoyote na kusisitiza: “Watanzania tusipelekwe kwenye mtego kwa kudharau vyombo vya usalama kwa sababu vimeihami nchi katika mazingira magumu na kuifanya iendelee kuwa na amani na utulivu.”
“Niwahakikishie, wale waliotumwa na wanaomezea mate rasilimali za Tanzania, tutailinda Tanzania na
rasilimali zake kwa gharama yeyote, watameza mate mpaka yataisha na wala Tanzania haitaendeshwa kwa rimoti,” aliongeza Dk Mwigulu.
Vilevile, Dk Mwigulu alisema yeyote anayetamani rasilimali za Tanzania moja ya eneo ambalo anatamani kuliharibu ni kwa Watanzania kutokuwa na imani na vyombo vyao.
“Tukatae jaribio lolote linalotuelekeza kuharibu uchumi wetu kwa sababu leo hii kama sio vyombo vya ulinzi na usalama nchi ingekuwa na hali mbaya,” alisema.
Aliwataka Watanzania kuwa kitu kimoja na kuzuia jambo kama hilo lisitokee na kwamba dawa ya jambo baya ni kutoruhusu jambo hilo kutokea tena.
Kadhalika, aliwataka Watanzania kuwa walinzi wa nchi yao kwa kutowafumbia macho watu wanaokuja katika nyumba zao huku wakiwa na malengo maovu.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
UMENIFURAHISHA SANA DR MWIGULU KUMBE NA NINYI MNAJUA NJAMA ZAO LENGO TUENDDELEE KUWAELIMISHA WATANZANIA WALIONE HILO !!!!!!!!