Aliyemdhalilisha kijinsia mgonjwa afukuzwe kazi

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ameagiza kufutwa kazi kwa daktari aliyekuwa akimtibu msichana mwenye umri wa miaka 18 aliyekuwa na tatizo la uzazi kwa kumdhalilisha kijinsia baada ya kumchoma sindano ya usingizi Urambo wilayani Tabora.

Agizo hilo amelitoa Leganga wilayani Arumeru mkoani Arusha wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua maeneo yaliyoathirika na vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu, Dk. Mwigulu amesema daktari huyo alipomaliza kumsikiliza mgonjwa huyo alimdanganya mgonjwa kwa kumchoma sindano ya usingizi na alipokuwa katikati ya sindano hiyo ya usingizi alimdhalilisha kijinsia.

“Mgonjwa alikwenda na mume wake, daktari akamsikiliza akamdanganya kwa kumchoma sindano na kumbaka lakini mgonjwa aliamka usingizi ila alibakwa na daktari huyo, haya ni mambo ya hovyo sana,” alisema Dk Mwigulu.

Amesema nesi alishuhudia tukio hilo na madaktari wengine wameshuhudia na wamethibitisha kuwa daktari huyo alimbaka msichana huyo na ameagiza muhusika anyang’anywe leseni. “Huyu akamatwe na asiachiwe,” alisema Dk Mwigulu na amemuelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, amfukuze kazi.

Amesema kama mtumishi huyo alisoma kwa mkopo au kwa kodi za Watanzania, wizara ya elimu ifuatilie afilisiwe na fedha hizo zirudishwe kwani Watanzania walitoa kodi zao asome lakini yeye kafanya unyama pia wanaotoa ithibati za madaktari wafuatilie ili anyang’aywe leseni yake.

Aidha amesema katika jambo hilo maabara nyingine wasijaribu kufanya kosa hilo kwani mambo hayawezi kuruhusiwa. Amesisitiza kila mtendaji na kiongozi serikalini afuatilie yanayoendelea katika taasisi mbalimbali zilizo chini yake.

Pia ametoa pongezi kwa viongozi wa mkoa kwa kuliona na kuchukua hatua, hivyo alisisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa nidhamu na wale wazembe watachukuliwa hatua. SOMA: …Aagiza Polisi wasimtafute Askofu Gwajima

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. WHATSAPP ☎️+254706758878 ☎️ ZUNGUMUZA NA MIMI MGANGA MKU WAGANGA WA MITISHAMBA HAPA KENYA NA EAST AFRICA.

    1. I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…

      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button