Nyuki wageuzwa kisima cha mapato, uhifadhi mazingira
MANISPAA ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma ina simulizi nzito ya mizinga 78 ya nyuki inayohusu hatua za ujasiri na ndoto iliyojengwa kwa tofali moja moja hadi kufikia mafanikio ambayo yamekuwa mfano wa matumaini kwa vijana wengi nchini.
Hii ni simulizi ya vijana sita katika Mtaa wa Masigara, Kata ya Shule ya Tanga, Songea wanaofuga nyuki na kuvuna si tu asali, bali pia kipato, heshima na matumaini mapya kwa kuwa kwa mwaka wanaingiza hadi Sh milioni 18 kutokana na asali.
Hivi karibuni katika jioni moja tulivu gazeti HabariLEO linakutana na mmoja wa vijana hao Dickson John, kijana mwenye tabasamu la kujiamini. Anaweka wazi kuwa safari yao haikuwa rahisi, lakini ilikuwa yenye maono.
“Tulianza mwaka 2016 tukiwa vijana wanne tu. Maisha yalikuwa magumu, ajira hakuna, lakini tulijua lazima tubuni njia sahihi ya kujitegemea,” anasema Dickson na kuongeza kuwa, sasa kikundi hicho kimeongezeka hadi kufikia vijana sita na hata kipato chao sasa ni kubwa kuliko walivyowahi kuwazia.

Katika mazungumzo hayo, Dickson John ambaye ni Katibu wa Kikundi anakumbuka kuwa, mwanzoni kikundi hicho kilianza na mizinga ya mbao mfumo ambao umetumika kwa mamia ya miaka, lakini wakabaini changamoto zinakuwa nyingi.
“Mizinga ya mbao ilikuwa ya gharama kubwa, haidumu na mavuno yake ni madogo. Tulivuna lita tano hadi saba tu kwa msimu kutoka mzinga mmoja,” anadokeza.
Utafiti mdogo, majaribio na kushauriana na wataalamu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ukawapa wazo jipya; kujenga mizinga ya tofali na kuezeka kwa bati mfumo ambao ni imara, wa kudumu na unaovutia nyuki zaidi na kwamba, hatua hiyo ilibadili kila kitu.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti HabariLEO, kutokana na hatua hiyo sasa katika mzinga mmoja wa tofali, wanapata lita hadi 25 za asali kwa msimu mavuno ambayo ni zaidi ya mara tatu ya mavuno ya zamani. Kimahesabu kwa wastani katika msimu mzima, mizinga yao 78 inawapatia hadi pipa tatu za asali. Pipa moja lina wastani wa lita 200 hivyo kupata wastani wa lita 600 kwa msimu.

Kwa hesabu za kifedha, lita 600 kwa Sh 10,000 kila lita ni jumla ya Sh milioni sita kwa msimu mmoja. Kwa kawaida, mwaka huwa na misimu mitatu hivyo kipato chao kinafikia wastani wa Sh milioni 18 kwa mwaka hivyo kwa vijana hao, huo si tu mradi, bali ni ajira halisi.
TFS wanawasha mwanga mpya
Ushirikiano wao na TFS hauwezi kupuuzwa. Dickson anasema, “Mizinga ya TFS inavutia nyuki sana. Rangi na muundo wake unafanya makundi ya nyuki kuhamia kwenye mizinga yetu. Hata makundi kutoka mizinga yao yanahamia kwetu kirahisi.”
Kisha Dickson anasema bayana kuwa, TFS hawakutoa tu elimu kwao, bali pia walitoa mizinga 20, saruji na msaada wa mara kwa mara wa kitaalamu. Mhifadhi ambaye nu Meneja wa TFS Wilaya ya Songea, Isa Mlela anathibitisha kuwa, lengo la TFS ni kuendeleza vijana katika sekta ya ufugaji nyuki.
Mlela anasema, “Tunawasaidia kwa kuwapa elimu, vifaa na mbinu bora za ufugaji ili waweze kuinua uchumi wao. Ufugaji wa nyuki ni fursa kubwa yenye tija na inayolinda mazingira.” Imebainika pia kuwa, ufugaji huo unavuka faida za kimapato kwani asali si faida pekee, bali pia kuna suala la faida kutokana na uchavushaji unaoongeza mavuno ya wakulima.
Hii ni kwa kuwa eneo la Masigira limepuliza uhai mpya. Mashamba ya alizeti, maparachichi na mazao mengine yanachanua kwa wingi kutokana na uwepo wa nyuki wengi katika mizinga hiyo ya Masigira. “Nyuki wetu wanaenda kufanya uchavushaji, hivyo wakulima wanavuna vizuri zaidi kuliko ilivyokuwa zamani kabla ya kuwapo mizina hii,” anasema Dickson.
Kimsingi, sasa wakulima wanapanda kwa wingi wakijua nyuki ni ‘wafanyakazi wa kimyakimya’ wanaoongeza uzalishaji wa mazao kati ya asilimia 30 hadi 60 kulingana na tafiti za kitaifa.
Utunzaji wa mazingira
Mbali na ufugaji nyuki, Kikundi cha Masigira Songea kinapanda miti ya kivuli, matunda na kutunza vyanzo vya maji. Kwao, mazalia ya nyuki ndiyo uhai wa mizinga.
Mazingira bora yana maana ya mavuno bora kila mwaka na ndio maana wanatumia taji mdogo, lakini wanapata faida kubwa Katibu huyo wa kikundi (Dickson John) anasema mizinga ya tofali haiozi, inadumu kwa zaidi ya miaka 20 na gharama zake ni nafuu ukilinganisha na mizinga ya mbao.
Kuhusu safari ya kuanzisha ufugaji wa nyuki, inaelezwa kuwa kijana anayetamani kuiga mafanikio ya vijana wa Masigira Songea, mifano yao ni mwongozo mzuri. Kubwa na la msingi ni kuwapo kwa nia thabiti na kisha, chagua eneo sahihi lenye miti na maua ya kutosha.

Eneo hilo liwe mbali na kelele au shughuli za binadamu. Nyuki hupenda amani na mazingira ya asili. Imebainika kutoka vyanzo mbalimbali kuwa, hatua nyingine ya msingi ni kuifunza ili usiingie katika ufugaji wa nyuki bila utaalamu.
Vijana wa Masigira Songea walifanya makosa ya mwanzo, lakini walijifunza kutoka kwa TFS na kwa majaribio yao ambayo yamewaletea mafanikio makubwa. Vifaa muhimu kwa kijana anayetamani kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki kwa faida ni pamoja na mizinga (tofali, mbao au kisasa), vifaa vya kuvunia asali, barakoa (maski),
glovu na vyombo vya kuchuja na kuhifadhi.
Chanzo kinasema ni muhimu kuanza polepole na kisha kuongeza hatua kwa hatua. Kinasema, “Hata mzinga mmoja unaweza kuleta faida ikiwa unatunzwa vizuri. Unapopata uzoefu, ongeza mizinga mingine kumbuka maisha ni hatua na kisha tafuta masoko mapema.”
Zingatia kuwa, ubora ndio siri ya kuvutia wanunuzi wengi wa bidhaa zitokana nazo na mazao ya nyuki ambayo yanahitajika katika masoko ya ndani, viwanda vya vipodozi na tiba asilia, maonesho ya kilimo na hata soko la kimataifa.
Ndoto hazijakamilika
Kwa mujibu wa Dickson, licha ya mafanikio waliyopata vijana hao wa Masigira, bado kuna njozi walizojisemea tangu mwaka 2016 za kujenga mizinga 100.
Hadi sasa wamejenga 78, lakini hawajakata tamaa. “Mfuko ulikuwa mdogo, lakini safari bado inaendelea. Tumefika mbali na tunaamini tutafika zaidi,” anasema Dickson kwa matumaini huku akiwatia moyo vijana wengine nchini kuwa na moyo wa ubunifu na uthubutu.
Anasema ufugaji wa nyuki umewaepushia hali ya kutangatanga mtaani hadi kuwa wakufunzi wa jamii. Wanatoa elimu, wanatunza mazingira na zaidi ya yote, wamejenga ajira yao wenyewe. Simulizi ya vijana wa Masigira wilayani Songea si tu habari ya mizinga na asali, bali ni simulizi ya uthubutu, ubunifu na nguvu ya kijana anayeamua kusema: “Sitasubiri ajira, bali nitaijenga.”
Vijana wengi nchini wanakabiliwa na changamoto za ajira na uchumi. Mfano huu wa vijana wa Masigira unathibitisha kwamba, mara nyingi suluhisho lipo kwenye ardhi,mazingira na maarifa. Ukitunza asili, asili inakulipa zaidi.




I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com