Acer yajikita kwenye vifaa vya teknolojia Afrika Mashariki

DAR ES SALAAM: ULIMWENGU wa teknolojia umeendelea kuibua mbinu na vifaa vipya ili kuruhusu dunia kutambua thamani na ukubwa wa teknolojia zinazoendelea kuvumbuliwa kwa manufaa ya jamii, Afrika na dunia.

Teknolojia hizo zinaweza kutumika katika bunifu mbalimbali, burudani na hata kuondoa vizuizi vya mawasiliano kwa kutumia suluhisho zinazobadilika.

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Teknolojia ya Acer Inc, Grigory Nizovsky ameeleza hayo wakati akizungumzia upanuzi wa soko la bidhaa hiyo Afrika Mashiriki.

Licha ya upanuzi huo kulenga mahitaji ya kibiashara, pia inalenga elimu. matumizi ya nyumbani na michezo ya mitandaoni.

Acer imejipambanua kama mshirika wa maendeleo ya elimu kwa kutoa vifaa kama Chromebooks, kompyuta mpakato na projekta zinazowezesha mazingira ya kujifunza kidijitali.

Kaulimbiu yao – “Kuondoa vizingiti kupitia teknolojia” – inaakisi dhamira ya kampuni katika kukuza ujumuishaji wa kidijitali barani Afrika.

Katika safu mpya ya bidhaa Afrika Mashariki, Acer inazindua makundi matatu makuu: vifaa vya Biashara na Elimu kama Veriton Desktops, TravelMate na seva za Altos; kwa watumiaji wa kawaida – Aspire, Swift, na vifaa vya Acer Connect; na kwa gamers – Nitro Series, Predator Helios na Triton, pamoja na Predator Monitors.

Acer pia inaleta safu ya Vero – bidhaa rafiki kwa mazingira zilizotengenezwa kwa plastiki iliyosindikwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni kupunguza utoaji wa hewa ukaa hadi kufikia kutokuwa kabisa na hewa hiyo ifikapo mwaka 2050.

Kampuni hiyo imetambuliwa kimataifa kwa juhudi zake katika uendelevu na usawa wa kijinsia, ikiwa ni miongoni mwa kampuni 10 bora katika Dow Jones Sustainability Index na kutajwa na Forbes kama moja ya Kampuni Bora kwa Wanawake Duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Kupitia mtandao wa washirika wa ndani, Acer inahakikisha upatikanaji wa bidhaa, huduma baada ya mauzo, mafunzo, na usaidizi wa kifedha katika ukanda huu. Kwa kuzingatia mafanikio ya kimataifa, kampuni inalenga kuleta suluhisho bunifu, nafuu n0a zinazofaa soko la Afrika Mashariki.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button