ACT Wazalendo wajitosa uchaguzi mkuu

ZANZIBAR: CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 16 na Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar.

“Kabla ya kufikia uamuzi huu, ACT ilifanya tafakuri ya kina na kujiridhisha kuwa huu ndio uamuzi sahihi unaopaswa kuchukuliwa na chama chetu,”
Kwa kuzingatia hali halisi ya kisiasa katika nchi na wajibu wa kimapambano amboa ACT Wazalendo imeubeba.”



