ACT-Wazalendo yajipanga kushiriki uchaguzi kwa amani

ZAZNIBAR; Chama cha ACT-Wazalendo kinaendelea kujiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa amani, licha ya kupinga kura ya mapema itakayofanyika Zanzibar siku moja kabla ya uchaguzi mkuu.

Akifungua kikao cha Kamati kuu ya chama hicho (Zanzibar), kinachofanyika Afisi Kuu, Vuga mjini hapa, Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Ismail Jussa, amesema chama hicho kinataka uchaguzi wa amani ili kushinda na kuunda serikali, huku kikihakikisha haki kwa watiania wanaowania uwakilishi na ubunge.

Jussa anasema chama chake kimeeleza wasiwasi wao kuhusu kura ya mapema kwa Rais Dk. Hussein Mwinyi na Rais wa Muungano Dk Samia Suluhu, ingawa hadi sasa hawajafanikiwa kuondoa kipengele hicho.

Amewataka wafuasi kuendelea kukiunga mkono chama hicho ili kuleta mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, huku Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikitarajiwa kuanza kutoa fomu za wagombea AgostiĀ 28.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button