ADC yaahidi kuruhusu uraia pacha

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Allience For Democratic Change (ADC), Wilson Mulumbe ameahidi iwapo atachaguliwa kushika dora katika uchaguzi mkuu mwaka 2025 ataruhusu uraia pacha.

Mulumbe ametoa ahadi hiyo wakati akinadi sera kwenye mkutano wa kampeni katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro na kueleza kuwa serikali ya ADC itaweka mfumo rafiki kwa Diaspora kuchangia taifa.

Amesema mpaka sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi nne pekee kati ya nchi 56 barani Afrika ambazo hazijaruhusu mfumo wa Uraia pacha jambo ambalo linazuia watanzania wanaoishi nje kuchangia taifa. “Mimi nitaungana nan chi nyingine 52, Tanzania itakuwa nchi ya 53, kuweza kuwa na uraia pacha”, amesema Mulumbe. SOMA: ADC yaahidi magari ya visima kila halmashauri

Amesema kipingamizi cha uraia pacha nchini Tanzania kimefanya watanzania wanaoishi nje (Diaspora) kutoshiriki moja kwa moja kwenye shughuli za maendeleo hali inayorudisha nyuma ukuaji wa kiuchumi “Haya matatizo yamepelekea ndugu zetu waitelekeze nchi yetu, washindwe kutuma msaada wa miamala nyumbani badala yake  inakwenda kujenga nchi nyingine. “Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanatuma hapa nchini kiasi cha Dola Milioni 800, wakati Diaspora wa Kenya wanatuma kiasi cha Dola Bilioni 5.7 ambayo ni zaidi ya Dola Bilioni 4.9”, amesema Mulumbe.

Mulumbe amesema iwapo atachaguliwa atahakikisha kwamba watanzania wanaoishi nje ya nchi wanachangia taifa na kuliingizia taifa zaidi ya dola bilioni tatu. “Hii itasaidia hata kodi ziweze kupunguzwa na kuwasaidia watanzania wapate nafuu ya ulipaji wa kodi kwa sababu ya pesa  tutakazoingiza”, amesema Mulumbe.

Amesema mzigo wa kodi umesababisha wafanyabiashara wengi wachanga kupata hasara badala ya faida jambao ambalo linahitaji vyanzo mbadala vya mapato kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi. “Tunaomba mtuchague kwa sababu sera zetu sisi zinakwenda moja kwa moja kuleta ahueni ya Maisha na kuwapunguzia watanzania ugumu wa Maisha”, amesema Mulumbe.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button