AfDB yaipiga jeki TADB usimamizi wa vihatarishi vya mabadiliko ya tabianchi

DAR ES SALAAM — Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeunga mkono Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) katika kuimarisha uwezo wake wa kupima na kusimamia hatari za mabadiliko ya tabianchi kwenye shughuli za kifedha, hususan sekta ya kilimo.
Mradi huo wa miezi sita, ulioshirikisha pia Kituo cha Kimataifa cha Uhimilivu wa Tabianchi (GCA) na wataalamu wa kimataifa kutoka Adelphi, umeiwezesha TADB kuzindua zana za kwanza nchini kwa ajili ya kutathmini hatari za tabianchi na kufanya majaribio ya msongo wa kifedha (climate stress testing).
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuwasilisha matokeo ya mradi huo, Derek Apell, Mratibu wa AFAC kutoka AfDB, alisema hatua hiyo itachochea taasisi za kifedha na wakopaji binafsi kuwekeza zaidi katika miradi ya uhimilivu wa tabianchi.
“Kadri taasisi za fedha zinavyotekeleza hatua za kuchuja wateja kwa kuzingatia hatari za tabianchi, ndivyo zinavyowapa motisha wakopaji kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, jambo litakaloongeza uwekezaji katika uhimilivu barani Afrika,” alisema Apell.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege, alisema mradi huo ni hatua ya kihistoria kwa taasisi hiyo na kwa Tanzania kwa ujumla.
“Ushirikiano huu unatupa fursa ya kusimamia ipasavyo hatari za tabianchi katika sekta ya kilimo na kutuimarisha kama benki kinara wa maendeleo ya kilimo nchini,” alisema.
Msaada huo pia unahusisha mafunzo ya kutumia zana mpya za kuchambua hatari za kimwili na za mpito, na kutathmini athari zake kwenye mtaji, ukwasi na faida za taasisi.
Hawaii Abdulla, Afisa Mkuu wa Mipango Mkakati na Kiongozi wa Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi TADB, alisema msaada huo umefika wakati muafaka kwani sasa benki inaweza “kufanya wasifu wa wateja kulingana na hatari za tabianchi na kusaidia utekelezaji wa mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi.”
Zana hizo mpya zinajumuisha mifumo ya kutathmini hatari za kimwili (za haraka na za muda mrefu) pamoja na hatari za mpito, na kuonyesha namna zinavyoweza kuathiri mtaji, ukwasi na faida za taasisi za kifedha.
Kwa hatua hii, TADB imejipambanua kama benki ya kwanza nchini kufanya tathmini kamili ya hatari za tabianchi, na kuwa mfano wa kuigwa kwa taasisi nyingine za kifedha barani Afrika.
F*ckin’ remarkable issues here. I’m very satisfied to see your post. Thanks a lot and i am having a look ahead to touch you. Will you please drop me a mail?
lways i usеd tto read smaller posts that as well clear their motive, and that is also happening with this ρost which
I am reading at tһis time.
Looк аt my web blog: Informasi24
Its like you read my thoughts! You appear to grasp a lot about this,
like you wrote the e-bookin it or something.
I believe that you can do with a few p.c. to drive the message home a
bit, however instead oof that, that is magnificent blog.
A fantastic read. I will certainly be back.