Ajali yaua wawili na kujeruhi 50 Pwani

PWANI: Watu wawili wamepoteza maisha akiwemo mtoto wa miezi sita na wengine hamsini kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya basi ndogo aina ya tata liliokuwa inatoka Kigogo Dar es Salaam kuelekea Mloka Rufiji kupitia njia ya Kisarawe kupinduka na kutumbukia mtoni.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge alipofika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kuwapa pole na kuwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Kisarawe amethibitisha vifo vya watu hao na kupokea idadi ya majeruhi 50 ambao kati yao saba wamekimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Baadhi ya majeruhi walionusurika katika ajali hiyo akiwemo mama mzazi aliyefiwa na mwanae wameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi wa dereva.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema ilihusisha gari lenye namba za usajiri T.275 DRZ iliyokuwa ikitokea Kigogo kwenda Mloka Rufiji.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button