Ajinyonga baada ya kufeli kidato cha nne

GEITA: BINTI mmoja mhitimu wa kidato cha nne, Rabia Paulo ,19, mkazi wa barabara ya Msalala, kata ya Kalangalala Wilaya ya Geita amejinyonga baada ya kufeli mtihani wa kidato cha nne.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuelezea kuwa tukio lilitokea Februari 11, 2025 majira ya saa 10 jioni.

Amesema binti huyo ni mhitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Nyanza iliyopo Manispaa ya Geita ambapo alipata matokeo kinyume na matarajio yake baada ya kupata divisheni sifuri.

Advertisement

Amesema tangu Januari 26, 2025 baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne 2024 kutangazwa na Baraza la Taifa la Mtihani (NECTA) aliapatwa ghafla na msongo wa mawazo uliopitiliza.

“Alisikia mama yake akimuelekeza dada yake marehemu kwamba aende akaangalie matokeo ya kidato cha nne ya mdogo wake na aliposikia alienda kujifungia chumbani wakajua tu amepumnzika.

“Lakini baadaye ilikuja kugundulika kwamba alikuwa amejinyonga na kwamba marehemu alikuwa anajua kwamba amepata matokeo ya divisheni sifuri, kwenye matokeo yake ya kidato cha nne”, amesema.

Kamanda amewaomba wazazi na jamii kwa ujumla kujenga ukaribu na watoto kwa kuzungumza na juu ya changamoto walizonazo ili kuepuka taharuki ya matukio ya watoto kuchukua maamuzi magumu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *